Bukobawadau

KIKUNDI CHA WATOTO ''THE MOST WANTED STREET DANCE PORTSMOUTH UK'' CHATOA MCHANGO KUSAIDIA WATOTO WENZAO BUKOBA

Kikundi cha Watoto '''MTOTO NI MALEZI'' wakiwa katika picha ya pamoji na Walezi wao nje ya Bango la Kanisa Mt.Yohanne Maria Muzzeeyi Parokia ya Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba muda mchache kabla ya hafla fupi ya makabidhiano ya Mchango walioupokea kutoka kwa kikundi cha Watoto wenzao cha 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk'
Carly-Ann Purcell na Kelly-Marie Baker pichani ambao ni walezi na walimu wakikundi hicho waliandaa Family Fun Day na kukaribisha Wasanii wengine maarufu kufanya maonyesho pamoja na michezo mbali mbali. Wenyeji na wafanya biashara wa mji wa Portsmouth waliweza kutoa michango yao.Kikundi cha ''THE MOST WANTED STREET DANCE PORTSMOUTH UK"kiliamua kati faida iliyopatikana isaidie watoto wenzao wa Bukoba. Sehemu ya mchango wamepewa watoto yatima wa Uyacho Hamugembe Rosemary Visram aliwaombea Utoto Mtakatifu Maruku msaada ambao umewakilishwa na Mzee Kabakaki wa Maruku Bukoba.
Muonekano wa Jengo la Kanisa la Parokia ya Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba.
Pichani kushoto ni Mzee Kabakaki akikabidhi  mchango huo kwa Padre Herbaert Muyelero ambaye ndiye paroko wa Kanisa la Mt.Yohanne Maria Muzzeeyi la Maruku .
FR.Herbaert Muyelero kushoto akipokea bahasha yenye Mchango wa shilingi shilingi milioni moja (1m.) mchango huo uliotolewa na Kikukundi cha watoto cha  ''THE MOST WANTED STREET DANCE PORTSMOUTH UK'' na kukabidhiwa siku ya Juzi Dec 1,2016 na Mzee Kabakaki.
 Kikundi cha Watoto '''MTOTO NI MALEZI'' katika picha ya pamoji na Walezi wao nje ya Bango la Kanisa Mt.Yohanne Maria Muzzeeyi Parokia ya Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba.
Walezi wa Kituo cha Watoto hao na Paroko wa Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba wakifurahi kwa pamoja

 Fr. Herbert Muyelero wakati akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa mchango huo.
 Barua ya Shukrani kutoka kanisa la Mt.Yohanne Maria Muzzeeyi Parokia ya Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba.
'Watoto wa kituo cha Maruku' wakifurahi kwa pamoja kufuatia mchango waliopata kutoka kwa Watoto wenzao wa Kikundi cha 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk'
Watoto hao wakiimba na kucheza nyimbo mbalimbali za kumtukuza Bwana.
 Pichani kutoka kushoto ni Matidia Kakoka na Generoza Amarungi ambao ni Walezi wa watoto na mwishoto kulia ni Mr. Ferdinand Nshange Katibu wa Parokia Maruku  Jimbo Katoliki la Bukoba.
Kutoka UK ni baadhi ya Watoto wanaounda kundi cha 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk'
Mmoja ya wanakundi la 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk' akitoa burudani

 Kikundi cha 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk' wakiendelea kutoa burudani Jukwaani na kupata fedha zilizoweza kutolewa kwa kikundi cha watoto wenzao wa Maruku Bukoba

 Onyesho maalumu kutoka kwa kundi la ''THE MOST WANTED STREET DANCE PORTSMOUTH UK'' lililopelekea Wenyeji na wafanya biashara wa mji wa Portsmouth kutoa michango ambapo sehemu ya Mchango huo uliweza kusaidia kituo cha watoto Yatima cha Uyacho kilichopo Hamugembe Bukoba na sehemu nyingine imeweza kuwafikia watoto wa  Kikundi cha''MTOTO NI MALEZI''kilichopo Maruku Bukoba.
 Wanaonekana pichani baadhi ya Watoto wanaunda Kundi la'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk'
 Photo Credit @Rosemary Visram
Bunners (mabango) ya kikundi cha 'The Most Wanted Street Dance Portsmouth Uk'
Next Post Previous Post
Bukobawadau