TAMASHA LA SIFA ZA YERIKO ARUSHA
Miaka 25 ijayo,
Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii
inamaanisha nguvukazi kubwa itakuwa mikononi mwao. Lakini kama watasalia kuwa
idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa
kwa ukuaji wa nchi.Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye
makusanyiko ya kijamii
mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa
nguvu. Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi
nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo
yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja
wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na
ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.
Uwepo wa Tamasha
la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation
Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha
kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya
changamoto kwenye jamii.Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha
watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za
watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine
ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa
wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali
maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono
Foundation.
Tamasha la Sifa za
Yeriko msimu wa kwanza inatarajiwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2016 Jijini
Arusha kwenye Kanisa la New Life City Church (Kwa Egon) lililoko Kwa Iddi, na
kisha kufuatiwa na Tamasha la pili litakalofanyika tarehe 11 Disemba Kanisa la
Tanzania Assemblies of God CCC Upanga Jijini Dar es Salaam ikiwa ni weekend hii.
Tamasha hili litahusishwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania, ambapo ugeni kutoka
Afrika Kusini utakuwepo. Wageni hawa ni Mercy Manqele, KgotsoMakgalema na
Sipokazi Nxumalo.Baadhi ya waimbaji wa ndani ni kama vile, Abednego na The
Worshippers, Toddlers International, Yusuphu Nahashon, Kwaya ya Uinjilisti
Kijitonyama,Wengine ni Machalii wa Yesu, The Cahogoz, Voice of Joy, Lilian
Kimola, na Bomby Johnson.
LENGO
Lengo la awali
nikukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zitatumika
kutafuta eneo la
kituo kwa jijini Dar es Salaam na Arusha, pamoja na matengenezo iwapo
itanunuliwa nyumba na kuibadilisha kuendana na maono ya jinsi kituo tunavyotaka
kiwe kukidhi mambo mbalimbali yatakayokuwa yakipatikana kituoni, kama kujifunza
muziki, uimbaji, ushauri nasaha, na utafutaji wa shule za kukuza vipaji ndani
na nje ya nchi.ambayo tunatarajia yatawezesha kupatikana kwa kiasi hiki ni kupitia
barua za mwaliko kwa watumishi mbalimbali wa dini na taasisi, pamoja na
kiingilio kitakachopatikana kupitia matamasha yote mawili.
GHARAMA
Ili lengo la
kukusanya milioni 200 kutimia, gharama mbalimbali kutoka kwa waanzilishi na
marafiki zimefanikisha katika kuwakaribisha waimbaji hawa kutoka Afrika Kusini,
kulipia mahala watakapofikia, matangazo, usafiri wa ndani, chakula, vyombo,
muziki na gharama nyinginezo. Hili litasaidia katika ukusanyaji wa kiasi
kilichosalia kwa awamu tofauti tofauti. Tunaamini katika ushirikiano katika
kutatua matatizo yaliyomo kwenye jamii yetu
Katika Kufanikisha na maono ya kupata fedha katika Tamasha hilo kwa Dar es salaam na Arusha kutakuwa na Kiingilio katika Matamsha hayo,Arusha ni Ijumaa hii Dec 9 pale kwa Egon Wakubwa 5000 VIP 20000 Dar es salaam ni Jumapili hii Dec 11 pale CCC Upanga Opp Chuo cha Mzumbe Watoto 5000 Wakubwa 10000 VIP 30000
Tunategemea support yenu wadau wa vyombo
vya habari Bloggers kwa kwa ajili ya kusaidia kutangaza Tamasha hili
linalofanyika lengo na maono tuliyo nayo mbele yetu Arusha na Dar es salam kwa
wikendi hii.