UNFPA YAKABIDHI MAJENGO YA DAMU SALAMA NA VIFAA TIBA ILI KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOANI KAGERA
Na: Sylvester Raphael
Wananchi Kagera sasa kunufaika na huduma ya Damu Salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera mara baada ya jengo la kuhifadhi Damu Salaama (Blood Store) kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa uongozi wa hospitali hiyo chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa.
Jengo hilo pamoja na jengo la Stoo ya vifaa tiba (Dry Store) yaliyojengwa kwa msaada wa Shirika la Kimataifa la UNPFA (United Nations Population Fund) na kugharimu jumla ya shilingi milioni 155,673,981/= yalikabidhiwa Desemba 20, 2016 na mwakilishi wa UNPFA Dk. Rutasha Dadi ambaye aliyakagua majengo hayo na kuridhishwa na viwango vya ujenzi wake.
Mara baada ya kukabidhiwa majengo
hayo mawili Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa alisema kuanzia sasa
katika hospitali hiyo tatizo la ukosefu wa Namu Salama litapungua kwa kiwango
kikubwa baada ya jengo kukamilika aidha litasaidia pia hospitali zote za mkoa
wa Kagera.
“Hapo awali tulikuwa tuna chumba
kidogo sana cha kukusanyia na kutunza damu salama kwa ajili ya wagonjwa wenye
uhuhitaji ambapo kilikuwa hakiendani na mahitaji ya hospitali yetu, aidha
tulikuwa na stoo ndogo ya vifaa tiba hasa tulikuwa tunapata shida kubwa ya
kutunza chanjo za aina mbailimbali lakini sasa majengo hayo yatatufaa sana.”
Alifafanua na kukushukuru Dk. Thomas
Aidha Dk. Thomas alilishukuru
shirika la UNFPA kupitia mwakilishi wake Dk. Rutasha Dadi na kuomba shirika
hilo liendelee kufadhili zaidi miradi mingine ya afya katika Mkoa wa Kagera ili
kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Majengo hayo yamejengwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na yameanza kutumika mara moja baada ya
kukabidhiwa rasmi.
Katika hatua nyingine wadau mbalimbali wameendelea kutoa misaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani hapa ambapo Kampuni ya kutafuta mafuta na gesi kwenye kina kirefu cha bahari (Orphir Enery) ilitoa tani 103 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 32 na Shirika la Kikristo YMCA Tanzania walitoa saruji mifuko 636 na mabati 214.
Vilevile Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Sokoine SUASA (Sokoine University of Agriculture Academic Staff Association) walitoa mifiko 200 ya saruji na missada hiyo yote ilipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kagera.