Bukobawadau

BAADHI YA VYANZO VYA MAJI VYAKAUKA KAGERA

Picha kutoka Maktaba Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akizungumza na mwananchi wa kata Mabale aliyefika kuchota maji katika bwawa la maji la Akashwa lililo kata Mabale. Bwawa hilo limekauka kwa kiasi kikubwa kutokana na kukosekana mvua kwa muda mrefu. Balozi Kamala ametembelea pia mabwaya ya Nyankere na Lwoga ambayo yako hatarini kukauka kama mvua hazitanyesha ndani ya kipindi kifupi kijacho.
Na Mwandishi wetu
Bukoba
MIRADI  tisa ya vyanzo vya maji katika wilaya nne za mkoa wa Kagera vimepungukiwa maji kwa asilimia kubwa hali inayofanya wananchi wa wilaya hizo kupata maji kwa mgao na wengine kuyafuata umbali mlefu.
Kauli hiyo ilitolewa na Mhandisi wa mkoa wa Kagera Vitus Exsavery wakati akiongea na Gazeti hili , alisema kuwa katika vyanzo ambavyo ni rasmi na visivyo rasmi upande wa vijijini vimekauka na baadhi vimepunguza maji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Hata hivyo Exsavery alisema,upungufu wa upatikanaji maji kwa wananchi hao kunasababisha kupata maji kwa mgao ni baada ya lita zilizokuwa zikihudumia kwa masaa 24 kutokuweza kutoka tena kutoka na vyanzo kubaki na lita za mgao wa masaa.
"Mpaka sasa tuliamua kuwagawia maji kwa masaa , kwa mfano lita 18000 zilikuwa zikitoka kwenye chanzo chenye uwezo wa kugawia zaidi ya vijiji vitatu nyakati hizi maji yanatoka kidogo sana yasiyoweza kuwagawia wote kama ilivyokuwa imezoweleka"alisema Exsavery

Alisema, wilaya ambazo zimepungukiwa maji kabisa ni kati ya wilaya ya Biharamulo, ambayo ilikuwaa na chanzo cha bwawa kimoja kilichokuwa kikihudumia wakazi wote kimekauka na kubakiwa na tope.

Aidha alisema kuwa, wilaya Bukoba ilikuwa ikihudumia vijiji vitatu cha Bonakilovyo,Kitaya, Kabumbilo, kutoka kwenye chemichemi kusambaza katika vijiji hivyo imepungua kwa kiwango cha asilimia 80 wananchi hupata maji kwa mgao.
Alieendelea kusema kuwa Manispaa ya Bukoba yenye kuhudumia kwa aina mbili ambapo baadhi ya kata hupata maji kutoka mamlaka ya maji safi na taka (Buwasa) na kata nyingine ambazo zilikuwa hazijafikwa maji hupata katika miladi ya chemichemi imepungua kwa asilima 40

Pia alisema katika miradi miwili iliyojengwa kwenye Kata ambazo hazipati maji ya Buwasa hutoa maji katika vyanzo vya kijiji cha Bunkango kilichopo Kata ya Nshabya na Bulibata ambao hutoa maji kwenye chanzo cha Nyamganja.
Aliongeza kuwa wilaya ya Muleba yenye vyanzo vitatu vya chemichemi vimepunguza kutoa maji kwa kiwango cha asiliia80 na Wananchi hutumia njia mbadala kupata maji ya kuweza kuhudumia kaya zao.
Aidha alisema upungufu wa maji kwa upande mwingine hufanywa na Wananchi wenyewe wanapokuwa wakifanya shughuli za kibinadamu kikiwemo kilimo karibu na vyanzo vya maji nayo ni moja kati ya sababu za kuchangiwa.

"Utamukuta mtu amelima ndani ya mita 60 au kutengeneza mitalo ya kutililisha maji karibu na vyanzo na kama kuna miti imekatwa anachoma nakusababisha kuupoteza uoto wa asili ambao ndio unalinda maji hayo" alisema Exsavery
Mwisho.

Next Post Previous Post
Bukobawadau