BALOZI KAMALA ATEMBELEA MABWAWA YA MAJI YA KATA MABALE - MISSENYI
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akizungumza na mwananchi wa kata Mabale aliyefika kuchota maji katika bwawa la maji la Akashwa lililo kata Mabale. Bwawa hilo limekauka kwa kiasi kikubwa kutokana na kukosekana mvua kwa muda mrefu. Balozi Kamala ametembelea pia mabwaya ya Nyankere na Lwoga ambayo yako hatarini kukauka kama mvua hazitanyesha ndani ya kipindi kifupi kijacho.