HOSPITALI YA RUBYA YAHITAJI FEDHA KUPANUA WODI YA KUJIFUNGULIA WAJAWAZITO
Picha
ya Pamoja ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rubya , wawakilishi wa shirika
la Jhpiego na Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilaini
baada ya kupokea tuzo na cheti kutoka shirika hilo.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Rubya Dr George Kasibante akionesha Cheti baada ya kukipokea kutoka shirika la Jhpiego chini ya mradi wa huduma ya mama na uhai wa mtoto Mkoani Kagera kwa kutimiza vigezo ya wizara ya afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
SR Theonestina John Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rubya akionesha tuzo iliyotolewa kwa Hospitali hiyo kutoka shirika la Jhpiego mkoani kagera kutokana na utendaji bora wa kutoa huduma ya mama na mtoto
Mganga mkuu wa Hospitali ya Rubya Dr George Kasibante akionesha Cheti baada ya kukipokea kutoka shirika la Jhpiego chini ya mradi wa huduma ya mama na uhai wa mtoto Mkoani Kagera kwa kutimiza vigezo ya wizara ya afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
SR Theonestina John Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rubya akionesha tuzo iliyotolewa kwa Hospitali hiyo kutoka shirika la Jhpiego mkoani kagera kutokana na utendaji bora wa kutoa huduma ya mama na mtoto
MULEBA:Na
Shaaban Ndyamukama
Kiasi cha Sh 200 milioni zinahitajika kwa ajili ya
ujenzi wa wodi ya akina mama
wanaojifungua katika Hospitali ya Rubya wilaya ya Muleba mkoani Kagera ili kupunguza msongamano wa wajawazito katika
Hospitali hiyo huku wengine wakijifungulia kwenye wodi za kulaza watoto wachanga.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Rubya Dr George
Kasibante amesema hayo leo wakati akitoa
taarifa ya utoaji huduma za mama na mtoto kwa shirika la Jhpiego na
kwamba wanaofika kujifungua Hospitalini hapo ni kati ya 300 hadi 360 kila mwezi badala ya120 na baadhi yao wanalala wawili katika kitanda
kimoja
Dr Kasibante alisema hayo katika kupokea tuzo ya
utoaji bora wa huduma ya mama na mtoto iliyotolewa jana na Shirika la Jhpiego mkoani Kagera na
kwamba kipindi cha miezi sita kati ya
June hadi Desemba 2016 wamejifungua wanawake 2,057 na baadhi yao hupelekwa wodi za watoto ili wasijifungulie chini
Alisema
Hospitali hiyo inapokea akina mama wajawazito kutoka maeneo mbalimbali
ya wilaya ya Muleba na baadhi yao hukaa kati ya siku saba hadi mwezi mmoja ili wapate huduma bora ya uzazi
wakati wa kujifungua.
Pia alisema wanawake wanofika kujifungua hufikishwa
kwenye jengo la muda lililojengwa kwa miti na kuzungukiwa mabati ambapo
hukumbwa na changamoto ya joto na msongamano ikiwa ni pampoja na kuhofia
kuambukizana magonjwa.
“Wanawake hao baadhi hujifungua watoto njiti ambao
uongozi wa Hospitali licha ya kuwa na upungufu wa wauguzi umejitahidi kuwatunza
watoto hao na kuokoa maisha yao na kuendelea kuishi wakiwa na mama zao”.Alisema
Dr Kasibante
Afisa Mipango wa Shirika la Jhipiego kupitia mradi
wa Mama na uhai wa mtoto mkoani Kagera Bi Alphonciana Barongo amesema licha ya
changamoto za Hospitali ya Rubya, shirika hilo linaipatia tuzo na cheti kwa
ajili ya utoaji huduma bora za afya na kupunguza vifo vya mama na watoto.
Alisema Shirika la Jhipiego kupitia mradi wa Mama na
uhai wa mtoto mkoani Kagera katika
wilaya ya Muleba mradi huo unahudumia Hospitali tatu za Rubya Kagondo na
Ndolage, vituo vya afya vitano na zahanati saba na kwamba Hospitali ya Rubya
imefikisha vigezo vya tuzo kwa kufikisha asilimia 85
“Wizara ya Afya
imekuwa ikitumia vigezo vya Tathimini kila kituo chenye mradi wetu kwa
kuangalia utoaji wa huduma na upungufu wa vifo vya mama na mtoto hivyo uongozi
wa Hospitali uongeze bidii kuhudumia wananchi” Alisema Barongo
Hata hivyo Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba
Methodius Kilaini ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya afya hospitalini hapo amesema
wafanyakazi na watumishi wanatakiwa kufanya kazi na kulinda maadili yao na
kwamba wasiowajibika wataondolewa ili
kuepuka kuchafua sifa ya Hospitali hiyo
Alisisitiza watumishi kufanya kazi kwa kutanguliza
uaminifu upendo na maadili mema katika kuhakikisha wanawafariji wanaokuwa na
changamoto za afya na kutumia fursa za zinazotolewa na mashirika ama serikali
kuwajibika ipasavyo.