Bukobawadau

MBARONI KWA KUMPIGA RISASI MFANYAKAZI WAKE

MBARONI KWA KUMPIGA RISASI MFANYAKAZI WAKE

Na Mwandishi wetu 
Bukoba.

MENEJA wa kampuni inayojihusisha na usambazaji wa bia Tanzania  Tanzania Breweries Limited (TBL) ya Global agency Arobogasti Byenobi (48) anashikiliwa na jeshi la pilisi mkoani kagera kwa kosa la kumpiga mfanyakazi wake kwa lisasi.

Hayo yalibainishwa jana na kamanda wa jeshi lapolisi mkoani Kagera Augustine Ollomi wakati alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mjini Bukoba.

Hata hivyo Kamanda Ollomi alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 10 january mwaka huu majira ya saa nanae na nusu mchana katika maeneo ya Ghara la kutunzia bia liliropo jilani na ziwa victoria katika manispaa ya Bukoba.

Alisema kuwa aliepigwa lisasi ni  Deogratia Didasi (25) chini ya  goti kwenye msuri ambapo lisasi hiyo ilikwama kwenye mguu na ilitolewa baada ya kufikishwa katika  hospitali ya mkoa. 

Ollomi alisema kuwa silaha hiyo imekamatwa na kukutwa na lisasi mbili tu ambapo 'Tumemuweka chini ya ulinzi kutokana na matumizi mabaya ya silaha na atafikishwa mahakamani.

"Katika hali ya kawaida sio vizuri bosi kupigana na kibaruwa wake pasipo kosa lolote na hata kama kungekuwa na kosa si vema kutumia silaha kinyume cha utaratibu na hairuhusiwi"alisema Ollomi

Pia wakati huo huo kamanda huyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa mmiliki halali wa siraha hiyo.

Aidha alisema kuwa mtu yeyote anapotaka kumiliki silaha anatakiwa kuwa amefikisha umri ya miaka 18 na unatakiwa kutoa sababu ya kumiliki siraha.

#BukobawadauMedia

Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau