PRESS RELEASE - AIRTEL MONEY YAGAWA FAIDA KWA WATEJA LEO
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango
wa kugawa faida ya Airtel Money unaofanywa na Airtel kuwafaidisha wateja
wake kwa kurudisha faida
walioitengeneza ndani ya huduma ya Airtel Money. Kulia ni Meneja wa
huduma ya Airtel Money bw Moses Alphonce. Hafla ya kutangaza mgawo huo
imefanyika leo katika ofisi za Airtel.
Meneja wa huduma ya Airtel Money Moses Alphonce akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa faida ya Airtel Money unaofanywa na Airtel kuwafaidisha wateja wake kwa kurudisha faida walioitengeneza ndani ya huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Meneja wa huduma ya Airtel Money bw Jackson Mmbando. Hafla ya kutangaza mgawo huo imefanyika leo katika ofisi za Airtel.
Meneja wa huduma ya Airtel Money Moses Alphonce akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa faida ya Airtel Money unaofanywa na Airtel kuwafaidisha wateja wake kwa kurudisha faida walioitengeneza ndani ya huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Meneja wa huduma ya Airtel Money bw Jackson Mmbando. Hafla ya kutangaza mgawo huo imefanyika leo katika ofisi za Airtel.
Airtel yagawa faida ya shilingi milioni 3.5 kwa wateja wa Airtel Money
Dar es salaam,
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airte leo imetangaza kuanza kwa mgawo wa faida yao wanaoipata kupitia
huduma ya Airtel Money ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.5 zaitagawiwa
kwa wateja wake.
Faida ya Airtel Money
inayogawiwa itawafaidisha wale wote wanaotumia huduma hiyo wakiwemo
wateja, wachuuzi wadogo na wakubwa (wakala) kuanzia leo. Mgawo wa faida
hiyo utategemea sana na salio la fedha ambalo
mteja atakuwa amepitisha kwenye akaunti yake ya Airtel Money kwa kipindi
cha robo ya mwaka.
Akiongelea kuhusu
utaratibu wa ugawaji wa faida hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema “ Hii ni mara ya nne toka Airtel Tanzania ilipoanza
kulipa faida ya Airtel money kwa wateja wetu pamoja
na wakala wote nchini, hadi sasa tokea kuanza kwa utaratibu huu kwa
ujumla tayari tumeshagawa zaidi ya bilioni shilingi 11.8 TZS tokea
tulivyoanza kufanya hivi mwezi Desemba mwaka 2015”.
Airtel tunajisikia
fahari sana kutangazia uma wa watanzania leo hii kwamba wateja wetu kwa
mwezi wa Junuari watapokea faida hii ili iwasaidie kufanya mambo mengi
hasa tukiamini kuwa huu ni mwezi mgumu kama
unavyotajwa na jamii.
Dhamira yetu iko pale pale tunawapa wateja kila mmoja sawasawa na
kiwango chake alichoweza kupitisha kwenye akaunti yake ya Airtel Money
kisha ataitumia atakavyo kulingana na mahitaji yake”
“Huduma yetu ya Airtel
Money imekuwa sana kutokana na wateja wetu kuitumia mara kwa mara.
Airtel Money kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi katika na
kusaidia maeneo mengi nchini ambayo hayajafikiwa
na huduma za kibenki. Airtel tunachukua nafasi hii kuendelea
kuwahamasisha wateja wetu wa Airtel Money kuendelea kuiamini huduma yetu
na kuitumia kikamilifu katika mambo mbalimbali yanayohusiana na malipo
ya pesa za kimtandao ili waendelee kujipataia faida
kubwa wakati wa mgao wa faida tunayogawa kila ifikapo robo ya mwaka”
alimaliza kusema Mmbando