MKASA HUU NI FUNZO KWA WAKIMWENGU
YAWALIMWENGU
Jamaa alimpigia simu rafiki yake:
"nina shida ya fedha rafiki yangu, mama yangu ni mgonjwa na sina hata senti kwa ajili ya matibabu yake"
rafiki yake akamjibu " nimekusikia rafiki yangu mpenzi, nipigie baadae kidogo tujue nini tunafanya"

jamaa alimpigia rafiki yake akiwa kahamanika kutokana na maradhi ya
mama yake, ila simu ya rafikie alikuta imezimwa. alipiga na kupiga
lakini hali ilikuwa vile vile.
ilibidi atoke nje kwenda kusaka ni mtu wake gani wa karibu anayeweza kumsaidia kwa ajili ya matibabu ya mama yake, lakini hakufanikiwa.
alirudi nyumbani akiwa mnyonge na kwenda moja kwa moja kitandani alipolala mama yake na kwa mshangao mkubwa akakuta mfuko uliojaa dawa mbali mbali kwenye kijimeza pembeni ya kitanda.
alimwita mdogo wake na kumuuliza kuhusu zile dawa:
"alikuja rafiki yako akachukua vyeti aliondoka navyo na baada ya muda ndio alirudi na dawa hizi zote, tulimpatia dawa mama pamoja na kaondoka punde tu hivi na kasema atarudi tena baadae"
jamaa alitabasam machozi yakimtoka machoni mwake, hakusubiri, alitoka nje kumfata rafiki yake na haikuchukua muda alimuona:
"ulikuwa wapi? nakupigia simu imezimwa nilikuwa nishapanik!"
rafiki alijibu: "ilibidi niuze simu yangu, baada ya kukosa fedha nilizotegemea kwa ajili ya matibabu ya mama, nilipokuja nyumbani na kukukosa ndio nikachukua juhudi ya kwenda kununua dawa kabisa"
Mmmhh! .... je mimi na wewe tunaweza kuwa marafiki wa aina hii? ...
Tujiulize nafsi zetu .... Inafundisha kidogo
Niwatakie siku njema,je wewe moyo huo....