Bukobawadau

RAIA WA BURUNDI ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA

Na Mwandishi wetu.
Kyerwa.
RAIA wa Burundi mkazi wa Bujumbura anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa kosa la kumugonga mwendesha pikipiki na pamoja na ambiria wake.
Kauli hiyo imebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Augustine Ollomi wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba.

Hata hivyo alisema kuwa Raia huyo wa Burundi aliefahamika kwa majina ya Pruzandekwe Thomas (49) alikuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T252AIT alipokuwa akitoka Rutunguru barabara ya kutoka murongo kwenda Kaisho majira ya saa 12 :15 mwaka huu.
Kamanda huyo alisema kuwa waliogongwa katika ajari hiyo na kupata majeruhi ni mwendesha pikipiki Ageti Gabriel (28) aliyekuwa amembeba Grolias Telesphory (15) mwanafunzi wa kidato cha kwaza waliokuwa wamepanda pikipiki nyenye namba ya usajiri MC698 BJU.

Alisema majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Nyakahanga iliyopo wilayani Karagwe ambapo wanaendelea na matibabu.
Wakati huo huo Kamanda Ollomi alisema kuwa watu watatu wamefariki dunia kwa nyakati tofauti wakiwemo wawili katika Wilaya ya Kyerwa na mmoja kutoka manispaa ya Bukoba.

Kamanda Ollomi alieleza matukio yalitokea mnamo tarehe 15 Jan,2017 kwa kusababishwa na Gari dogo aina ya Toyota Primoo namba ya usajiri T686 BHN lilokuwa likielekea Kimuli kutoka mabila lilimgonga Swamadu Swaibu Myambo mtoto aliekuwa anasoma darasa la pili nakupelekea kifo chake.

Dereva wa gari hiloalitokomea kusiko julikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi.
Mauwaji mengine yalitokea katika kitongoji cha Chanya tarafa Nkwenda Fransisi Majura Muhaya (83) mkulima mkazi wa chanya aliuwawa kwa kupigwa fimbo kichwani na vipande vya matofari ya kuchomwa na kuvuja damu nyingi sana na kusabasha kifo chake.
Kamanda Ollomi alisema kuwa husika wa tukio hilo ni mtoto wa marehemu Atugonza Gerevazi (21) alikuwa anampiga baba yake Domisian Gerevazi (78) baada ya majirani kuja kuwaamua ugomvi huo ndipo kijana huyo alipo muacha baba yake na kuanza kumshambulia.
 
Ruta Reonadi (45) mkazi wa Nyamukazi muhaya mvuvi aliokotwa akiwa amefariki maeneo ya kata kashai matopeni akiwa anatokwa na damu sehemu za masikioni na puani .
Aidha alisema kuwa mwili huo umetambuliwa na ndugu na sasa upo katika Hospitali ya rufaa ya mkoa Kagera.
MWISHO.
Next Post Previous Post
Bukobawadau