Bukobawadau

SBL yawapatia Watanzania milioni mbili maji ya uhakika, salama

 Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi  kwa  waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia watanzania milioni 2 katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo  inayolenga kuboresha maisha katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema jana  katika hoteli ya Morena Mkoani Dodoma.


Waandishi wa habari wa mkoani Dodoma wakichukua matukio wakati wa mkutano uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena mkoani Dodoma.

Moja ya mradi wa maji uliodhamiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited  uliozinduliwa mapema Novemba mwaka jana katika Kijiji cha Makanya wilayani Same katika  programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo  inayolenga kuboresha maisha.




Dodoma, Januari 24, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi ya  milioni mbili kote nchini maji safi na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita  kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo  inayolenga kuboresha maisha.

 Kupitia programu yake inayofahamika kama Maji kwa Uhai, SBL imechimba visima vya kisasa 16 katika mikoa minane na kuwezesha jamii  katika maeneo hayo  kupata maji ya uhakika na salama.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha  alisema kwamba kampuni hiyo ya bia  imejikita katika kupunguza uhaba wa maji katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitaabika kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

 “SBL  ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya Maisha  ikiwa ni moja ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu  imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua  maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Wanyancha aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji  kuliko kusafiri umbali mrefu  kutafuta maji.

Aliongeza, “licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya jamii  unahakikisha kuwa watoto hususani watoto wa kike  wanaosoma shule  wanapata muda  mzuri wa  kuhudhuria  shuleni kwa uhuru zaidi bila usumbufu”.

Mkurugenzi huyo wa Mahusiano  alieleza kwamba mpango wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni  kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha, Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha  wakazi zaidi ya 300,000.
Next Post Previous Post
Bukobawadau