SHIRIKA LA JHPIEGO LATOA TUZO ZA KAZI KWA WATUMISHI WA HOSPITALI WILAYANI NGARA
Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Nyamiaga Dr Simon Kyamwenge akipokea
cheti kama tuzo ya Hospitali baada ya kutimiza vigezo katika Mradi
wa afya ya mama na mtoto wa MCSP wengine ni watumishi wenzake
wakishangilia kwa tuzo hiyo
Picha zote na Shaaban Ndyamukama kutoka wilayani Ngara .
Wauguzi ,Waganga pamoja na Madaktari wa hospitali za Rulenge na Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera wakiandamana kuelekea katika ukumbi kupokea tuzo ya utendaji kazi bora wa huduma ya mama na uhai wa mtoto ( MCSP ) kupitia shirika la Jhppiego mkoani Kagera

Wauguzi,waganga na madaktari wakiwa katika Picha ya pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama (mwenye suti nyeusi ) na Afisa mipango wa MCSP chini ya shirika la Jhpiego mkoani kagera Alphoncina Barongo jirani kulia mwa mkurugenzi
Hata hivyo Barongo amesema mkakati wa kutoa tuzo katika hospitali vituo vya Afya na zahanati ni kwa kila wilaya ambapo katika mkoa wa kagera ni vituo vya Afya 12 hospitali za wilaya na baadhi ya zahanati kuanzia Bukoba manispaa , Muleba , Biharamulo , Ngara , Karagwe , Bukoba vijijini na Misenyi
Dr Kyamwenge amesema hospitali hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya mama na watoto (wodi) wakati wa kupata huduma ya kujifungua ambapo chumba kilichopo kina uwezo wa vitanda vitatu vya kujifungulia badala ya sita, kuna chumba cha upasuaji chenye vitanda vinane badala ya vitanda 24
Ameongeza kuwa hospitali haina chumba cha kuhudumia watoto wachanga ambao huchanganywa na watoto njiti kwa kulazimika kulala na mama zao kwenye vyumba vyenye msongamano wa wagonjwa, na kwamba ili kukidhi mahitaji hayo zaidi ya shilingi milioni 400 zinahitajika kujenga vyumba hivyo.
Picha zote na Shaaban Ndyamukama kutoka wilayani Ngara .
Wauguzi ,Waganga pamoja na Madaktari wa hospitali za Rulenge na Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera wakiandamana kuelekea katika ukumbi kupokea tuzo ya utendaji kazi bora wa huduma ya mama na uhai wa mtoto ( MCSP ) kupitia shirika la Jhppiego mkoani Kagera
Wauguzi ,Waganga pamoja na Madaktari wa hospitali za Rulenge na Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera wakiandamana kuelekea katika ukumbi kupokea tuzo ya utendaji kazi bora wa huduma ya mama na uhai wa mtoto ( MCSP ) kupitia shirika la Jhppiego mkoani Kagera
Wauguzi,waganga na madaktari wakiwa katika Picha ya pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama (mwenye suti nyeusi ) na Afisa mipango wa MCSP chini ya shirika la Jhpiego mkoani kagera Alphoncina Barongo jirani kulia mwa mkurugenzi
Hospitali
ya Nyamiaga na Rulenge katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera zimepokea
tuzo kutoka shirika la Jhpiego baada ya kutekeleza mpango wa huduma ya
mama na uhai wa mtoto na kutoa huduma bora kwa walengwa baada ya
kutimiza vigezo vya wizara ya afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na
watoto
Afisa mipango
wa afya ya mama na uhai wa mtoto (MCSP) kupitia shirika la Jhppiego
mkoani Kagera Alphoncina Barongo, ametoa tuzo na vyeti kwa hospitali
hizo katika wilaya ya Ngara ambapo mpango huo unahudumia hospitali
tatu za Rulenge, Nyamiaga na Murugwanza, vituo vya Afya vitatu na
zahanati 12
Alphoncina
Barongo amesema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa serikali kuu,
halmashauri za wilaya pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya
Jhpiego ,JSI, Save the Children, lengo likiwa ni kupunguza vifo na
kutoa huduma bora ya afya ya uzazi na watoto wachanga chini ya miaka
mitanoHata hivyo Barongo amesema mkakati wa kutoa tuzo katika hospitali vituo vya Afya na zahanati ni kwa kila wilaya ambapo katika mkoa wa kagera ni vituo vya Afya 12 hospitali za wilaya na baadhi ya zahanati kuanzia Bukoba manispaa , Muleba , Biharamulo , Ngara , Karagwe , Bukoba vijijini na Misenyi
Kaimu
mganga mkuu wa Hospitali ya Nyamiaga Dr Simon Kyamwenge amesema pamoja
na kupewa tuzo hiyo na cheti bado Hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba
wa vyumba vya wagonjwa hasa wanawake wajawazito ambao hujifungulia
sakafuni kwa kukosa vitanda pamoja na changamoto ya kifedha ya ruzuku
toka serikalini
Amesema
Hospitaliya hiyo inakabiliwa na changamoto za utoaji huduma za afya
kwa wananchi ikiwa ni pamoja na uhaba wa fedha za ruzuku ya serikali (
OC) na kutegemea mapato ya mfuko wa bima ya Afya ya Taifa NHIF pia
fedha za papo kwa papo zitokanazo mfuko wa afya jamii CHFDr Kyamwenge amesema hospitali hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya mama na watoto (wodi) wakati wa kupata huduma ya kujifungua ambapo chumba kilichopo kina uwezo wa vitanda vitatu vya kujifungulia badala ya sita, kuna chumba cha upasuaji chenye vitanda vinane badala ya vitanda 24
Ameongeza kuwa hospitali haina chumba cha kuhudumia watoto wachanga ambao huchanganywa na watoto njiti kwa kulazimika kulala na mama zao kwenye vyumba vyenye msongamano wa wagonjwa, na kwamba ili kukidhi mahitaji hayo zaidi ya shilingi milioni 400 zinahitajika kujenga vyumba hivyo.
Pamoja
na hayo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama
ametoa wito kwa watumishi wa hospitali hizo kufanya kazi kwa kuzingatia
taratibu kanuni na sheria za utumishi ikiwa ni pamoja na kulinda maadili
yanayokubalika kijamii huku wakitoa lugha rafiki ya kuwawezesha
wagonjwa kupata matumaini ya kupona licha ya kuhitaji dawa na huduma
nyinginezo