Bukobawadau

SOCCER LA KULIPWA ULAYA NA AMERICA

Tukianza na mtiririko mzima kwa wanasoka wa Tanzania, wapo wachezaji ambao waliuchukulia mpira wa miguu ni kama moja ya starehe,Iwe labda kwa kupunguza vitambi,Pia wachezaji ambao walijitahidi kucheza mpira wakiwa na dhamira kubwa siku moja wapate angalu bahati waweze kucheza Simba au Yanga kwakuwa ndio vilabu vilikuwa vinaonekana angalau unaweza kuvaa vizuri na ukapata offer kuingia mziki bure na mambo Mengine ya hanasa,
Labda kwa wale wenzangu wa miaka ya 70, 80 mpaka 90, wanaweza kujitetea kwamba miaka ile soka walikuwa wanacheza kama mapenzi tu hakukuwa na motisha ya kumfanya mchezaji aone kwamba pale uwanjani ndio kazini na soccer ndio maisha yake yote.
Wadau wenzangu lazima mjue Mpira wa miguu ni Hazina kubwa sana,
wachezaji wa ki Tanzania wanatakiwa walitambue hilo,
Kwa mfano leo hii Mchezaji wa Tanzania nataka  nimlete Marekani aje kucheza Soccer, kutakuwa na changamoto kubwa  sana,Kwanza hautopata market nzuri, sisemi hivyo kwa kuwaponda wa Tanzania wenzangu la hasha,
Kila kitu kipo wazi, ukiangalia katika Link ya FIFA, Tanzania wapo katika nafasi ya 156, na Marekani wapo katika nafasi ya 28, ki soccer,  wakati ukiangalia majirani zetu Rwanda na Burundi ni nchi ambazo zimekumbwa katika mikasa ya kivita kwa muda mrefu,lakini leo hii wametuzidi katika Link ya FIFA. na mbali sana,Sasa utategemea vipi mchezaji wa Tanzania achukuliwe kama mchezaji wa kulipwa nchini Marekani, kwa kwenda kubadilisha kitu gani hasa katika soccer?
Mimi binafsi nawakubali wachezaji wetu wapo wazuri na ningependa kuwasaidia wakafika mbali
sana, 

Lakini mimi binafsi nakuwa na hofu kubwa sana hawatopata kile ambacho mimi nafikiria,
Mshahara mzuri,Marupurupu ya kutosha, Malazi.Chakula na Usafiri. Kwakuwa mimi ndio naweza kuwa mdhamini wake,Gharama zote hizo zitakuwa ni juu yangu,Sasa Klabu itakayo mchukuwa wata amuwa wamlipe Dolla 500, kwa mfano,
Mimi binafsi kama mfadhili wake sinto kubaliana na malipo hayo,matokeo yake Itabidi mcheza arudi nyumbani,Sina uhakika kama mchezaji huyo atalizungumza jina langu kwa wema,
kwa kuwa wa Handishi wa habari za michezo watependa kujua safari yake tangu ilipokuwa mwanzo mpaka ilipo fikia,siamini kama atakuwa mkweli 100% na hapo ndipo atakapo lichafua jina langu kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.

Ushahuri wangu tu kwa chama cha Mpira cha Tanzania kwanza kithamin mchango wa wachezaji kwani watambue bila wachezaji, wao kama viongozi wasingekuwa pale walipo.
awaondolee wachezaji vikwazo,

Na chama cha mpira kizingatie zile sheria 17 za FIFA,
Wakifanikiwa hilo basi watambue mpira wa Tanzania utafika mbali sana na watatambulika kwenye  medani ya soccer kimataifa.
Pia jambo kubwa ambalo mimi linalo nishangaza hasa kwa Vilabu vikubwa vya Tanzania kuchukua wachezazaji kutoka nje ya Tanzania kama wachezaji wa kulipwa,
Tujiulize wadau wenzangu,
Chama cha mpra kilitumia vigezo gani na kuwapa nafasi wao ya kuja Tanzania kucheza soka ya kulipwa?
Leo mchezaji wa Tanzania kupata timu ya nje ya Tanzania kuna  vigezo vingi vina hitajika, Kwanza awe na muonekano mzuri wa kimaumbile,
Na kama ni mfungaji basi ajue idadi ya magoli mangapi amesha funga, iwe kwa mechi za kitaifa kimataifa,
itakuwa vizuri zaidi angalau awe amesha chezea timu ya Taifa lake " National Team" na umri wake je utamruhusu?
Kwa sababu timu inapo mchukuwa inakuwa inafanya biashara watategemea kwamba watafanya mauzo ya Jezi kupitia mchezaji walio mnunua na sio kuja kucheza Nachi, 
Natumaini wadau wenzangu mpo na mmepitia Kila mstari katika haya niliyo jaribu kuwaletea.
Nawaombeni na nyinyi mchango wenu wa  mawazo  nini kifanyike ili niweze kusaidia wana Soccer wa Tanzania?
KAJU SPORTS BLOG.

Next Post Previous Post
Bukobawadau