AJALI YAUA WATU WANNE MJINI BUKOBA
WATU wanne wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajari ya gari iliyotokea kata Rwamishenye manispaa ya Bukoba mkoani Kagera
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi Augustin Ollomi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa hari juu ya tukio hilo. Hata hivyo alisema kuwa ajari hiyo ilitokea tarehe 24 mwaka huu majira ya saa 16 .30 jioni katika barabara ya Uganda maeneo ya Rwamshenye wakati gari lililosababisha ajali hiyo lilikuwa na no za usajiri T.377 BZW aina ya EICHE likiwa linaendeshwa na Josiah Joel Kasigwa (47) mkazi wa miembeni manispaa ya Bukoba. Aliwagonga waendesha pikipiki Damian Augustno (30) mhaya aliyekuwa na pikipiki namba MC .188 AZM aina ya bajaji boxer Denis (32) mhaya mkazi wa Rwamishenye alikuwa na pikipiki namba MC.582 aVQ aina ya Sanlg Alisema kuwa watembea kwa mguu waliogongwa ni Patricia Patrick (35) mfanyabiashra na mkazi wa Rwamishenye, Florence Innocent (28) nakusababisha vifo vyao papo hapo.
Tukio hilo Iilitokea wakati gari hilo lilipokuwa likitoka shule kuchukua wanafunzi na kuwapeleka majumbani kwao. Aliwataja majeruhi kuwa Jackson Sebastian (10) Leus Optati (12) Molin Sebastin (8) ,Johansen Chrizostom (11) Kelvin Clemence (9) ,Wema Idrisa (36) wate wanafunzi Aidha Ollomi alisema kuwa majeruhi hao wametibiwa na kuruhusiwa isipokuwa Jackosn Sebastian amelazwa na hali yake inaendelea vizuri, Na, mtuhumiwa amekamatwa na jeshi la polisi na chanzo cha ajali kinachunguzwa.
Naye Katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera Kilwanila Kaiza alikili kupokea miili ya watu wane waliopoteza maisha na kuhifadhiwa katika mochwali iliyopo katika hospitali ya Rufaa iliyopo mjini Bukoba.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajari hiyo rwehumbiza Belezeti ,atwaa mickdard alisema kuwa gari iliyosabisha ajari ni gari la shule ya msingi na awali ya kujitegemea Rwekiza. "Tuliona gari inakuja kasi Sana mi nikamwambia mwenzangu kuwa unaona ngoma hiyo toka toka tukakimbia Mara baada ya muda ikagonga mti wa mbele basi ikaanguka"alisema belezet "Sema tu watu sio wasikivu alipiga Sana honi lakini watu hawakujari wakaendelea tu kufanya mambo yao hadi gari inawafikia Walikuwa wamekaa ndo kufikia hali hiyo ilitokea"alisema mickdard.
Pata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD APP