DIWANI KIMWANI AAPISHWA NDANI YA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI MULEBA
Diwani wa kata ya Kimwani Wilayani Muleba mkoani kagera
Daudi Kiluma kupitia Chama cha mapinduzi ameapishwa leo na kupewa hati
ya ushindi wa kuwa diwani wa kata hiyo baada ya kushinda uchaguzi mdogo
uliofanyika januari 22 mwaka huu
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Chrizant Kamugisha amemtaka diwani
huyo kutumia uzalendo kuongoza wananchi wa kata yake bila kujali itikadi
za kisiasa katika kuhakikisha anasimamia maendeleo kupunguza changamoto
zinazowakabili
Kamugisha
(mwenye joho jekundu) amesema uchaguzi huo uliofanyika kimwani ulikuwa
wa amani na utulivu na kwamba kasoro zilizojitokeza hazikusababisha
uchaguzi huo kukwama na kwamba wananchi wanahitaji huduma bora za
kijamii kutoka kwa diwani Kiluma
Aidha
amesema viongozi wa CCM na halmashauri kwa ujumla watoe ushirikiano
katika kumuelekeza jinsi ya kusaidiana na wakuu wa idara kuwasilisha
changamoto za watu wake katika sekta ya afya elimu maji na mtandao ya
barabara bila kuacha mkakati wa kutunza mazingira
"Wilaya
yetu baadhi ya maeneo yanakabiliwa na upungufu wa chakula hivyo
madiwani tuhimize wananchi wetu kutumia mvua zinazoendelea kunyesha
walime na kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukosa kwa muda mfupi"
Alisema Kamugisha
Diwani
Kiluma akiapa mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Muleba
Cleophace Waane amesema atailinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania sheria za Tanzania maadili ya madiwani na kanuni za kudumu
kisha kutumikia wananchi kwa uhuru na usawa
Amesema
atashirikiana na madiwani wenzake na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Muleba kuwasilisha mahitaji ya wananchi wa kata
hiyo akianza na vipaumbele alivyojiwekea kutimiza ahadi zake wakati wa
kampeni alipokuwa akinadi Sera za Cha cha Mapinduzi
"Kwa
Wadhifa wangu wa udiwani nitahifadhi , nitailinda na kuitetea akiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utii uaminifu , kwa uwezo na uwezo
wangu wote ikiwa ni pamoja na kutekeleza kanuni za kudumu za halmashauri
hii ya Muleba " Alisema Kiluma
Uchaguzi
wa udiwani katika kata ya Kimwani Wilayani Muleba ulifanyika baada ya
aliyekuwa amechaguliwa mwaka 2015 Silvesta Faustine Muliga kupitia chama
cha Wananchi ( CUF) kuuawa mwaka jana na watu wanaosadikiwa
kutofautiana katika itikadi za kisiasa