Bukobawadau

JIUNGE NA 'GANYAMUKANDA SYNDICATE' WADAU WA MAENDELEO KATA YA KISHANDA MULEBA

 Wajumbe wa kamati ya shule ya msingi Ganyamukanda wakiwa na wawakilishi kutoka Ganyamukanda syndicate. Fatuma Abdallah na diwani Charles Kinubi
 Muonekano wa Chumba Kimoja cha Darasa ulioanzishwa  hapo awali na Wanaganyamkanda Mdau Cyprian Iraba na Balthazar Iraba Kufikia hapo pongezi kubwa kwao na tunawaomba wanakishanda na Wanaganyamkanda kuiga na kua na Utaratibu huu wa kujitoa kwa kuchangia Elimu na Sekta nyingine.
FURSA YA KUCHANGIA MAENDELEO:Ndugu zangu mliosomea Ganyamukanda, kuna group la whatsapp lililoanzishwa na Bwana Edmund Bejumla na kuitwa GANYAMUKANDA SYNDICATE tangu mwaka jana 2016,Tulianzisha group hili kwa lengo la kutoa tulichonacho kwa ajili ya shukrani kwa kuwa tumesoma Ganyamukanda na hatunabudi kuikumbuka shule yetu tulikotoka.
Kwa ujumla waanzilishi wa kundi hili walikuwa 21,kadri tulivyoendelea tumefikia wajumbe 32 mpaka sasa. 

Mpaka sasa 'Wanaganyamkanda' tayari wamatekeleza Mradi wa Ujenzi wa choo cha walimu matundu mawili ambacho kiligharimu takribani 3000000/=(milioni Tatu)
Na tunaendelea kuhamasisha ili tuweze kupata tank la maji ambalo litakuwa la lita 30000.
Tunaomba wana Ganyamukanda popote mlipo muweze kujiunga na group letu ili tuweze kuweka alama ya wanaGanyamukanda Alumni. Karibuni sana.
Admin mkuu      ; (Edmund Bejumla        0783240000
Admin msaidizi ; Madam Fatuma  Abdallah   0754656672

 Moja ya mafanikio ya 'Wanaganyamkanda' ni mradi wa Choo cha Walimu wa Shule ya Msingi Ganyamkanda.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Ganyamkanda akiongea na baadhi ya wanafunzi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau