MUSHEMBA TRINITY SCHOOL NI TUNDA LINALOCHIPUKIA KAGERA NA TANZANIA
Mushemba Trinity School Bukoba ni shule ambayo ilianzishwa mwaka 2012 ikiwa na watoto 26
hasa wenywe uitaji katika jamii lakini pia kutoka katika familia za
kawaida, ni shule ya Bweni na kutwa, ila kwa sasa inapokea watoto
wasichana tu kwa ajili ya kulala kuanzia miaka 4 na kuendelea.
Kwa sasa Shule hii ina watoto 309 na ina darasa la watoto wadogo sana(baby class) Pre.school, darasa la 1-5.Shule hii ni English medium ambayo mkazo wake ni kutumia kingereza na inawalelea watoto katika maadili ya kikristo.
Shule hii ni mojawapo ya miradi iliyoanzishwa ili kumuenzi Baba Askofu Dr.Samson Mushemba pichani kulia ambaye ni Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT NA ASKOFU wa DKMG
Shule
hii ilianzaishwa chini ya shirika la Mushemba Foundation, lenye makao
yake makuu Kagera Bukoba, chini ya mwanzilishi wake mkuu Bwana Josephat Mushemba ambaye amekuwa akiishi Denmark lakini akijithidi kuinua swala la elimu kwa watoto wa Kagera.
Madhumuni makuu ya shule ni kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wasiojiweza na wale wanaojiweza ili kuleta uwiano katika jamii bila kubagua mwenye uwezo na asiyena uwezo.
Kwa maana hiyo Mushemba Foundation inafadhili watoto karibia 130 wanaokwenda kwenye shule hii inayoitwa kwa kifupi MTS.
Wafadhili wa hawa watoto wanatoka hasa katika
nchi ambayo Josephat anaishi kule Denmark, ambao ni marafiki wake na
familia aliyonayo kule dk ni mtandao ambao JOSEPHAT ameujenga kwa miaka
mingi akiwa nchini.
Kila
mwaka Mushemba ufadhili asilimia 40-50 ya watoto wanaoingia shuleni na
asilimia zinazobaki ni watoto ambao wanachngia gharama za masomo.
Shuke hii ambayo kwa mda wa miaka michache Imeonyesha umahili
mkubwa wa kufundisha, walimu wake ni walimu ambao wanapewa training za
mala kwa mala , shule ambayo inapokea pia wageni na wafadhili kutoka
Denmark ambao uitembelea shule hii mala nyingi kwa mwaka , ambayo
uwafanya watoto wapate mda wa kuongea na kuuliza maswali na kujua
utamaduni mwingine.
Shule hii pia inajitahidi kufundisha kwa vitendo licha
ya madarasa yao kuwa katika uhodari wa juu sana lakini bado walimu
uchukua mda mwingine kuwatoa nje na kuwafundisha kwa vitendo.
Pamoja
na hayo shule hii imepata vifaa vyake vyote kutoka Denmark, kuanzia
viti meza, black boards kila kitu kimetumwa kutoka nje
Shule
inavifaa mbalimbali vya michezo na shule inasisitiza kwamba watoto
wapate mda kiasi wakucheza na vifaa mbali mbali kuburudisha akirim na
imeonyesha kuwajengea uwezo mkubw a darasani na kujiamini
Shule pia mwaka jana ilianziasha bustani kubwa inayowalisha watoto mboga za majani ambazo ni fresh, hii yote ni kuwajengea watoto lishe nzuri wawapo shuleni na kuweza kumudu masomo yao shuleni
Matokeo ya darasa la nne kitaifa yashanganza watu.
Mushemba Triniy school ambayo mwaka jana darasa
lake kwanza lilifanya mtihani wa kitaifa wa kuingia darasa la Tano,
matokeo yake yameshanganza watu wengi, Shule imekuwa ya 3 kiwilaya na 5
kimkoa na Ya 13 kitaifa, kwa matokeo haya shule imeonyesha umahili wake na kusaidia kupandisha mkoa wetu wa KAGERA KITAIFA PIA, wadau wengi wameipongenza sana shule.
Tarehe 7/2 shule ilifanya sherehe
kubwa siku nzima ambapo walimu walipewa zawadi na watoto wakasherekea
ushindi , mkuu Mkurugenzi wa Shule Bwa J osephat Mushemba na mke wake
LEA ALIKUWEPO KUWAKABIDHI zawadi walimu na baadae baba askofu mstaafu Dr
Mushemba aliongea na watoto na walimu. Ilikuwa ni sherehe iliyoambatana
na kwaya za watoto wa shuleni pamoja ngoma .
Shule ina na uwezo wa kubeba wanafunzi wengi na labda kujaza mpaka darasa la saba kwa sababu ya
facilities zilizopo lakini mkurugenzi wake amekuwa akikisiitiza hatupo
kwa ajiri ya kufanya biashara bali kuinua elimu na kuhakikisha tuna
fikia viwango.kwa sababu ya watu wengi kuipendelea shule , viongozi wa
shule wamekuwa wakiwassitizia wazazi wanaotaka wanafun zi wake kuja
Mushemba Foundation kuomba nafasi mapema sana kuliko kusubiri dakika za mwsiho,
Bibi
lena amabaye ni mratibu wa Mushemba Foundation amesema mwaka huu
wamerudisha waombi ya watu karibu 70 ambao walikuwa wameomba nafasi
za kujiunga na shule kuanzia january, anasema tumekuwa na wakati mgumu
kuwakatalia lakini hatukuwa na jinsi maana kiasi tulivhopanga kila
darasa kilikuwa kimetimiaDirector wa Mushemba Foundation Tanzania Mvh hilsen Josephat Mushemba pichani ambaye pia ni muanzili shi Mkuu wa Mushemba Trinity school bukoba akiwapongenza wanafunzi na walimu kwa matokea mazuri ya mtihani wa serikali walipofanya sherehe.
Walimu na wafanyakazi walioweza kupokea zawadi kwa ajili ya Ushindi shuleni hapo.
Baadhi ya watoto wakiwa darasani katika Majengo ya kisasa kabisa yaliyojengwa hivi karibuni.
Watoto na wafanyakazi wakisherekea ushindi kufuatia matokeo mazuri ya shule yao
Taswira baadhi ya Majengo ya Shule hiyo
Trinity School rised and became one of the Best Schools In Tanzania according to the latest national exams.
We are so proud of our pupils who worked so hard. Together with the teachers and all other workers at Trinity School we have managed to put Trinity School in a high position in the whole country.
We thank God and give him all the honour for that
DOWNLOAD Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD