RAPPER METTY MUBASHARANI NA DAYNA NYANGE KWENYE KWENYE WIMBO WA YOUR LOVE
Rapper Metty kutoka jijini Dar es salaam ametangaza kachia kibao kipya kinachoenda kwa jina la YOUR LOVE.
Wimbo
huo wenye mahadhi ya muziki wa kizazi kipya " bongoflava" maudhui
yalioambatana kuimba na kurap kiasi mtindo unaowavutia mashabiki wengi
wa muziki huo.
Katika
wimbo huo Metty amemshirikisha mwanadada Dayna Nyange anaefanya vizuri
kwenye medani ya muziki kwa sasa pamoja na muimbaji mwingine
anaechipukia kwa kasi aitwae Nappy.
Wimbo wa
YOUR LOVE umetengenezwa na mtayarishaji maarufu nchini Tanzania Mr T
Touch katika studio za Touchez Sound zilizopo sinza jijini Dar es
salaam.
Katika mahojjiano na mwandishi wa
habari hizi Metty amesema wapenzi wa muziki wakae mkao wakupkea muziki
mzuri wa level ya kimataifa,amejipanga vyakutosha na hivi punde ataachia
kibao hiko ambacho kitapatikana katika vyanzo mbalimbali ikiwemo
redio,lunimga na mitandao ya kijamii.