Bukobawadau

WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BANGI WILAYANI NGARA NA BIHARAMULO

Jeshi la polisi katika wilaya za Ngara na Biharamulo mkoani Kagera linawashikilia wakazi watano wa wilaya hizo kwa kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya Kulevya huku wakihusika kuharibu mazingira ya misitu.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao, ambao walikamatwa kwenye operesheni ya kukamata wanaojihusisha na kilimo cha bangi wiki hii pamoja na watumiaji au wafanya biashara wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Kagera
Kamanda Olomi aliwataja waliokamatwa kwenye wilaya hizo ni Fabian Kasigo (45), mkazi wa Kazingati, Ndaluhekeye Chiza (37),Nestory Kachukuzi 42), Renatus James (44) Khalid John (33) wakazi wa wilaya ya Ngara na James Maliatabu (35) mkazi wa kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele alisema katika msako wa kuwakamata wakulima wa bangi wilayani Ngara jumla ya mashamba ekari 20 yalibainika na wakulima wa zao hilo wanalilima katikati ya mapori wilayani humo
Mntenjele alisema wakulima waliokamatwa na kuhojiwa walidai wanauz zao hilo kati ya Sh15,000 hadi Sh 17 000 kwa wateja kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi na kwamba wanalima zao hilo wakikata miti kwenye vyanzo vya maji
“Wanapolima bangi wanaiweka katikati ya mashamba ya mahindi na huwezi kutambua kwani wanatembea umbali mrefu katikati ya mabonde yanye vyanzo vya maji na kukata miti kisha kupanda kupanda bangi hiyo”Alinema Kanali Mntenjele
Alisema katika msako uliofanyika kwa siku tatu wilayani Ngara kata ya Ntobeye, Keza kiasi cha ekari 20 zilibainika, wanaolima zao hilo wakiwatumia hata wahamiaji haramu kutoka mataifa jirani na wilaya hiyo wakiishi porini na kuletewa mahitaji ya chakula.
Aidha mkuu wa wilaya ya Biharamulo Saada Malunde alisema kata iliyofanyiwa msako kukamata wakulima wa bangi ni kata ya Nyantakara na Nemba ambapo mkulima mmoja James Maliatabu (35) alikutwa na shamba la bangi ekari 10.
Alisema vita ya dawa za kulevya kwa maeneo ya vijijini ni utumiaji wa bangi ambapo pia kamati za mazingira katika vitego na idara za halmashauri zinatakiwa kuunga mkono serikali kuwataja na kuwakamata wanaojihusiha na biashara ya madawa ya kulevya ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
Pia baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama katika wilaya hizo walishauri serikali za vijiji na madiwani hata maafisa kata na tarafa kufanya zoezi la kuwasaka wakulima wa bangi kila mahali ili kutokomeza madawa ya kulevya kote nchini.
 Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya ngara mkoani kagera ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Luteni Kanali Michael Mtenjele wakisafiri kwa pikipiki kuelekea kwenye mashamba ya kilimo cha bangi kata ya Keza tarafa ya Rulenge ambapo Jumla ya ekari 20 zimebainika na kukamatwa watu wanne wanaojihusisha na kilimo cha bangi katika mapori pamoja na misitu yaliyoko kitongoji cha Mulole kata hiyo ya keza 
Mwenye chupa ya maji na sweta la bluu ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama ambapo alilazimika kutambaa akishuka na kupanda milima kuingia ndani ya mashamba ya bangi 
Picha na habari by Shaaban Ndyamukama
 BOFYA HAPA KUDOWNLOAD BUKOBAWADAU APP Kwa habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store

Next Post Previous Post
Bukobawadau