Bukobawadau

WANAFUNZI YATIMA WASAIDIWA BAISKELI NA MADAFTARI KUHUDUMIA MASOMO WILAYANI NGARA

Mratibu wa Mfuko wa Tumaini ulio chini ya kanisa la Anglikana Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Alex Samoya Nyamkara, (kushoto) akiwakabidhi wanafunzi yatima wa  shule ya sekondari Rusumo  B wilayani  Ngara baiskeli zilizotolewa na wahisani kutoka nchini Canada na Uingereza hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi yatima wa shule ya sekondari Rusumo B Wilayani Ngara Mkoani Kagera wakionesha furaha yao baada ya  jana kupokea baiskeli kutoka kwa marafiki wa kanisa la Angilikana la wilayani humo ambao wanatokea nchini Uingereza na Canada.

Picha na Shaaban Ndyamukama

NGARA: Marafiki wa  kanisa la Anglikana wilayani Ngara mkoani Kagera, jana wametoa msaada wa baiskeli 13 zenye  thamani ya Sh2.08 milioni kwa wanafunzi  yatima wa shule ya sekondari ya kata ya Rusumo B, ili  kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwahi masomo shuleni hapo.
Mratibu wa mfuko wa Tumaini  Alex Samoya Nyamkara  alisema marafiki hao wanaotoka  nchini Kanada na kisiwa cha Gumsey cha nchini Uingereza ambao wanafadhili miradi  ya kijamii kupitia Mfuko wa Tumaini na kwamba pia wamekabidhi madaftari 1400 yenye thamani ya Sh1.6 milioni kwa wanafunzi 60 wa shule ya sekondari Rusumo B, Keza na Nyakisasa.
Nyamkara alisema kupitia wahisani hao  shule 22 za kata wilayani Ngara zimenufaika kwa kuboreshewa mazingira ya kufundishia na kujifunzia hasa kwa kujengewa matundo ya vyoo , matanki ya maji na  miundombinu mingineyo huku wanafunzi hao wakipatiwa taa za umeme wa jua (solar) ili kujisomea  usiku.
Alisema wanafunzi waliopatiwa baiskeli hizo huamka alfajiri kwa kutembea umbali wa kilomita saba kila siku   wakitokea nymbani kwao sawa na kilomita 14 kwenda na kutoka shuleni  ambapo nhuchelewa kuanza masomo na wengine hukatisha masomo yao kwa kukumbwa na vikwazo mbalimbali hasa wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito katika umri mdogo
Alisema katika shule ya sekondari ya Kabanga wanafunzi wanajengewa matundu 10 ya vyoo yenye thamani ya Sh.42 milioni, Shule ya sekondari Murugwanza wanajengewa matanki ya maji, na wanafunzi wanaofaulu kitato cha nne na cha sita ambao ni yatima wataendelea kupewa mikopo kusomea fani mbalimbali
“Kwa wanaojiunga na vyuo vya uuguzi na ualimu hao wanapewa mikopo asililimia 100 na wanarudisha baada ya kupata ajira na kuanza kujikimu pamoja na familia zao ili kuwawezesha kutokata tama ya kujiendeleza” Alisema Nyamkara

Aidha mkuu wa shule ya sekondari Kabanga Aaron Sekazoya alisema katika shule yake yenye wanafunzi  yatima 54 wanaofadhiliwa na Tumaini fund walioko kidato cha tano na sita wanapatiwa sh 120 kwa ajili ya ada ya mwaka na matumizi mengineyo, ikiwa ni pamoja na fedha za mitihani kwa kidato cha nne.
Pia wanafunzi hawa hujaza fomu maalum kwa ajili ya kutyaja mahitaji yao na hatimaye baadhi yao hupatiwa madaftari  sare za shule na taa za kujisomea kwa wanaotoka mazingira yasiyokuwa na nishati
Alisema shuleni kwake  kunafanyika ukarabati wa matanki mawili ya  maji  yenye ujazo wa lita 80,000 ili kukidhi mahitaji ya maji shuleni ambapo kwa siku   maji yanayotumika ni kati ya lita 3,000 hadi 4,000 na kwamba  shule hiyo itakuwa na  wanafunzi wa bweni na kutwa  936 iwapo wataripoti wote wa kidato cha kwanza
Wakizungumza na wanafunzi waliopokea msaada baikeli na madaftari  kwenye shule hizo marafiki wa kanisa hilo kutoka  kisiwa cha Gamsey  nchini Uingereza   Sofi Danford pamoja na Linda Wainy wa nchini Kanada waliwataka wanafunzi   kujifunza kwa bidii na kutimiza ndoto zao kupitia taaluma ya elimu.
Linda alisema pamoja na kuitembelea wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika shughuli za kichungaji bado watahitaji kusaidia katika sekta nyingine za kijamii kama kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuelekeza misaada kwa wanafunzi wa shule za msingi ambao baadhi yao wanakosa mahitaji katika familia.
Next Post Previous Post
Bukobawadau