TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ametengua rasmi
nafasi ya Mtendaji
Mkuu wa Shirika Elimu Kibaha Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za
kiutendaji zinazomkabili.
Akijibu swali la Waandishi
wa Habari waliotaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya tuhuma mbalimbali
zinazolikabili Shirika la Elimu Kibaha ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo
vya habari kwa muda mrefu sasa, Mhe. Simbachawene alisema kutokana na kuwepo
kwa tuhuma mbalimbali za uendeshaji, Mhe. Rais
Magufuli tarehe 4/3/2017 ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili
kupisha uchunguzi.
“ Ni kweli tuhuma juu ya
uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na
Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka
kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi
na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo
kwa hoja zinazohitaji uchunguzi
zaidi. Hivyo, ili uchunguzi huo uweze
kufanyika Mhe. Rais amemsimamisha kazi
Mtendaji huyu Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina
dhidi yake. Alisema Mhe. Simbachawene
Alisema uamuzi wa
kumsimamisha umechukuliwa kwakuwa tuhuma za awali zilizojitokeza dhidi yake
zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi.
Kwasasa nafasi ya Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Rebecca
Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini,
Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa.
06/03/2017.