UWANJANI KAITABA:SERENGETI BOYS 3 - 0 BURUNDI
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha na habari/ Faustine Ruta.
Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa KaitabaViongozi mbalimbali walikuwepo
Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys
Mgeni Rasmi na viongozi wengine wakisalimiana na Viongozi na wachezaji wa akiba wa Burundi
Nyimbo za mataifa yote mawili ziliimbwa kabla ya mechi kuanza
Taswira kabla ya mtanange
Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys
Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange
Picha ya pamoja
Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi. Picha na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara bila Kiingilio!!!
Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati
Kim na Bakary Shime wakiteta huku mtanange ukionekana kuwa mtelezo kwao kipindi cha pili katika mchezo wa karafiki leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Kocha Bakar Shime ataiongoza tena Serengeti Boys siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa pili.
Kipa hakuona kitu!
Nahodha wa Serengeti Boys Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mchezaji wa Serengeti Boys (kushoto) akipeta kwa bao lao la tatu
Bao tatu 3-0
Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati
Shangwe! 3-0
Chupuchupu afunge bao lingine!
Assad Ally Juma wa Serengeti Boys(kushoto) akiufukuzia mpira
Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni
Kibabane tena na mpira
Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi
Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja
Dakika 90 zilikamilika