UZINDUZI WA TOVUTI TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati
wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika Ukumbi wa HazinaMjini Dodoma jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizindua tovuti za
Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe. (Kushoto) ni Mwenyekiti
wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick wakifuatilia uzinduzi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja
na viongozi mbalimbali katika Mikoa na Halmashauri wakifuatilia uzinduzi wa
Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina.
Tovuti hizo zinalenga katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na
kwa haraka ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.
Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani wakati wa uzinduzi
wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika Ukumbi wa
Hazina mjini Dodoma.