PICHAZ + VIDEO: JUMA NATURE ASEPA NA KIJIJI DAR LIVE
Msanii Nguli wa Bongo Fleva, Juma Kassim 'Nature' akipanda jukwaani.
SHANGWE zilikuwa shangwe usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, namaanisha Dar Live ambapo wakali wa kudondosha utamu wa burudani, Juma Nature, Harmorapa, Msaga Sumu na wengine waliteka jukwaa kwa kuachia mangoma ya maana huku kuwaacha mashabiki zao waki-enjoy.
Nature akikamua jukwaani.
Katika shoo hiyo ya Usiku wa Pasaka, Msaga Sumu, Nature, Harmorapa walioneshana umwamba kwenye ishu nzima ya kukonga nyoyo za mashabiki zao.
Shoo ikibamba
Msaga Sumu kama kawaida yake na ngoma zake za uswazi, Singeli alikinukisha huku Nature akigonga zote kali za kitambo na mpya. Hakika watu walifurahi si kifani.
Harmorapa aliyekuwa akisubiliwa kwa hamu aliamsha homa ya burudani baada ya kupanda jukwaani na kushika maiki, wakti mashabiki wakiwa hawaamini kinachoendelea Mmakonde huyo aligonga burudani isiyo ya kawaida huku akiwaacha mashabiki midomo wazi na kushangilia kila dakika.
Burudani zikinoga.
Juma Nature 'akiliamsha dude'.
PICHA NA ISSA MNALLY | GLOBAL PUBLISHERS