Rais John Magufuli atoa zawadi za Pasaka kwa Makundi maalum
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
sista Stella Selugenge wa Kituo cha Kulelea watoto cha Msimbazi Center leo Jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
Bibi Veronika Msanjila wa Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge leo Jijini Dar es
Salaam.
(Picha zote
na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Anthony Ishengoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya
vituo 9 katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya
Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya
Mhe. Rais,Kamishna wa Ustawi wa jamii Bw. Rabikira Mushi amesema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa
kawaida kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kutoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia
ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu
kama ilivyo kwa watu wengine.
Akifafanua Mushi amesema Mikoa
ingine iliyofaidika na zawadi hizo ni Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga,
Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida,
Mwanza, na Pwani.
Aidha vitu vilivyofaidika na
zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao
ya Watoto Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha,Makao
ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.
Viuo vingine ni Makao ya Watoto
Yatima Group Trust Fund, Temeke.Makao ya Watoto Dar Al Arqum (International
Islamic Relief Organization),Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga,Makazi ya
Wazee Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge Kigamboni.
Kwa upande wa Zanzibar Bw. Mushi
alitaja Vituo vilivyonufaika na zawadi
hizo,Kituo cha Watoto Istima - Chakechake, PembaMakazi ya Wazee Wasiojiweza Sebleni
– Unguja.
Aidha kwa Mikoa ya Tanzania Bara
jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya Mhe. Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi,Makazi ya
Wazee Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro,Mahabusu ya Watoto Mbeya,Mahabusu ya
Watoto Arusha,Mahabusu ya Watoto Tanga,Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzage Tanga,Makazi
ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.
Utoaji wa zawadi umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Waheshimiwa
Marais tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi za
vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi
na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.
Mwisho.