Bukobawadau

COSAD TANZANIA NA CLUB YA ROTARY BUKOBA WAKABIDHI MRADI WA MBUZI MMOJA KWA KILA MAMA (ONE WOMAN ONE GOAT) KAGONDO,BKB

COSAD Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Rotary International/Rotary Club of Minneapolis USA (Kupitia tawi la Rotary Club of Bukoba) wametembelea Mradi maarufu kama OWOG- One Woman One Goat (Mbuzi Mmoja kwa Kila Mama) wenye  lengo la kumkomboa  kila Mama kuondokana naUmaskini na kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyofikiwa.

UBUNUNIFU ULIOZAA MFANIKIO:  Akina Mama wanashauriwa kuwa kwenye kundi la kaya Kumi (10). Ukopehswa Mbuzi wa Maziwa kilamoja na kujengewa tanki la maji kila watu kumi. Na pia upewa Ushauri wa Kiufundi na Daktari wa mifugo kwa miezi 12 bure. Mama anapashwa kurudisha mbuzi jike baada ya Mwaka mmoja ili mradi uweze kusambazwa kwa akina Mama wengine.
MATOKEO (Award Winning Results): Mwaka Jana Mradi tayari Ukishinda Tuzo ya Kimataifa ya Rotary (Rotary Hero Award-2nd Run up) kutokana na Ubunifu huo. 
Zaidi ya kinamama 500 kutoka kaya mbalimbali maeneo ya Kagondo ,Izigo Wilaya ya Muleba, Bugabo na Kangabusharo(Bukoba Vijijini) wameishanufaika na mradi huo kwa kupata maziwa na kuzalisha mbuzi ambao soko lake lipo la kutosha kupitia wadau wa COSAD na Rotary (Mbuzi mmoja wa maziwa huuzwa kati ya 80,000-100,000/=) na hivyo kumfanya Mama kuwa na kipato cha uhakika. Lengo la COSAD ni kusambaza mbuzi 2000 kwa akina Mama Mkoani Kagera ifikapo 2020 na kumfanya kila mama mwenye nia kuishi maisha ya neema.
 Baadhi ya mbuzi hao wa Kisasa wanapatikana katika shamba la mradi lililopo Kagondo Manispaa Bukoba
 Mmoja waWanawake ambao ndio wanufaika wakubwa wa mradi huu akitolea jambo ufafanuzi.
 Bango lililopo katika shamba la mradi.
Prof Kilahama  akichukua picha katika moja ya banda la wafugaji wa mbuzi hao.
 Mzee Mashashi akibadilishana mawazo na mama ambaye ni mnufaika wa mradi maarufu kama OWOG- One Woman One Goat (Mbuzi Mmoja kwa Kila Mama) wenye  lengo la kumkomboa  kila Mama kuondokana naUmaskini
 Taswira wakati wadau wa Rotary Club of Bukoba na wadau wa Cosad wakitembelea kaya mbalimbali kujionea maendeleo ya mradi OWOG- One Woman One Goat (Mbuzi Mmoja kwa Kila Mama) wenye  lengo la kumkomboa  kila Mama kuondokana na Umaskini ambapo wameridhishwa na mafanikio ya mradi huo.
 Ukaguzi wa mradi ukindelea.
  Baadhi ya wanufaika wakiendelea  kutolea maelezo juuchangamoto wanazokumbana nazo.
 Baadhi ya Wanawake ambao ndio wamekuwa wakinufaika wakubwa wa mradi huu wa kijamii wa ufugaji mbuzi wa kisasa, wakitoa shukrani za dhati kwa Mr.Smart Baitani Rais wa Cosad Tanzania na Viongozi waandamizi wa Rotary Club of Bukoba
Unaweza kusoma zaidi kuhusu Mradi huu kupitia Tovuti ya COSAD: www.cosad.org 

Next Post Previous Post
Bukobawadau