UZINDUZI WA MRADI WA MAJI (ITOMA - KATORO) ULIOFADHILIWA NA BI ZAHARA ABDALLAH
Bi Zahara Abdallah pichani kushoto amefadhili kikamilifu mradi wa Kisima cha Maji katika Msikiti waTaawal uliopo Katika Kijiji cha Itoma Kata Katoro Bukoba Vijijini,Mradi huo umegharimu Shingi Shilingi Milioni 14,Maji ya kisima hicho yatasambazwa pia maeneo ya Jirani na Msikiti huo Kijijini hapo,Mradi huo umezinduliwa na Alhaji Sheikh Hashim Hassa Kamugunda (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamu Shafiim Mkoa Kagera na makamu Mwenyekiti Taifa waislamu madhehebu Shafii (R.A),kulia kabisa ni Ndugu Abdulrazak Dattan mme wa Bi Zahara ,tukio lililofanyika Siku ya Idd Mosi June 26,2017 na kuhudhuriwa na mamia ya waumini.
Mgeni Rasmi Alhaji Sheikh Hashim Hassa Kamugunda ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamu Shafii Mkoa Kagera na makamu Mwenyekiti Taifa waislamu madhehebu Shafii (R.A) akikata utepe kuzindua Mradi wa Kisima cha Maji kwenye msikiti wa Taawal uliopo Itoma-Kata Katoro,mradi huo umefadhiliwa na Bi Zahara Abdallah (wapili kutoka kushoto).Maji hayo yanatalajiwa kusambazwa maeneo ya Jirani kijijini hapo.
Bi Zahara Abdallah akiomba dua na kumshukuru Allah mara baada ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Kisima cha maji ikiwa ni hatua ya pili ambapo mapema mwezi April aliweza kujitolea na kuwajengea waumini wa Kiislam wa Itoma -Katoro msikiti ikiwa ni baada ya ule wa awali kuathirika vibaya kufuatia tetemeko la ardhi lililotekea,September 10 2016 Mkoani
Sehemu ya Waumini waliohudhuria Uzinduzi wa Kisima hicho sambamba na kushiriki Shughuli maulid ya Balaza la Idd lililofanyika Siku ya Idd Mosi June 26,2017.
Kisomo cha kumsalia Mtume Muhammad (s.a.w)
Neno kutoka kwa Mgeni Rasmi Alhaji Sheikh Hashim Hassa Kamugunda Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamu Shafii Mkoa Kagera na makamu Mwenyekiti Taifa waislamu madhehebu Shafii.
Sheikh Faharu Musthapha akimpongeza Mgeni Rasmi mara baada ya kutoa neno
Ustaadh Hassim Bin Juma akikabidhi lisawa kwa Mgeni Rasmi
Meza Kuu yupo Alhaji Sudi Fresh,Sheikh Faharudin na wengineo #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Burudani ya Mchezo wa Sarakasi ikiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Katoro Islamic wakitoa burudani ya Mchezo wa Sarakasi
Umati wa watu ukifuatilia burudani zinazoendelea wakati wa Sherehe za Maulid ya Idd.
Sehemu ya wakazi wa Vijiji vya Jirani na katoro wakifatilia kinachojiri katika shughuli hiyo
Vijana wa Kikundi cha Dufu kutoka Itoma-Katoro wakiwajibika.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Katoro Islamic wakiwa katika picha ya pamoja na Bi Zahara Abdallah.
Bi Zahara katika picha ya pamoja na wanafunzi wa madarasa ikiwa ni mlezi wao.
Muondelezo wa matukio ya picha #bukobawadau #balazaLaIdd-ItomaKatoro
Umati wa wanaweka waliohudhuria tukio hilo wakifatilia kwa makini kinachoendelea #bukobawadau #balazaLaIdd-ItomaKatoro
Mwanafunzi wa Madarasa Fatuma Binti Hamduni akistoa kisa cha Mtume Muhammad(swalla Allahu alayhi wasallam
#bukobawadau #balazaLaIdd-ItomaKatoro
Hajjat akishindwa kujizuia na kuungana na watoa burudani ya Dufu.
Taswira meza Kuu wakati shughuli ya Maulid ikiendelea
Wanafunzi wa madarasa ya Itoma wakishusha burudani ya Dufu kama utakavyoweza kujionea kupitia akaunti yetu ya Youtube @bukobawadau
#balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Utapata kuona yote yaliyojiri kupia akaunti yetu ya You tube #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Burudani ya Dufu
Kinachoendelea ni burudani ya Dufu #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Baadhi ya Viongozi wa Dini waliowedha kushiriki shughuli ya Maulid ya Baraza la Idd El Fitri na Uzinduzi wa kisima cha maji.
Kwa dhati kabisa Bi Zahara pichani na mme wake Abdulrazak Dattan wakitoa shukrani zao kwa wananchi wa katoro kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuupata, ambapo pia wametumia fursa hiyo kuendeleza kuwa wataendelea kusaidia jamii ya wanakatoro kwa kadri mungu atakavyowajilia.
Neno la Shukrani kutoka kwa Bi Zahara Abdallah likiendelea...
Miongoni mwa vijani wawili waliosilimu wakiombewa Dua kwa Unyenyekevu.
Muendelezo wa matukio ya picha #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Bwana Abdulrazak Dattan akitoa zawadi kwa Vijana Mwesiga Geofrey na Mwesiga Alfred walioamua kusilimu na Sasa majina yao ni Rasheed na Ibrahim.
Alikadhalika Bi Zahara akitoa chochote kwa Kijana Mwesiga Geofrey na Mwesiga Alfred waliosilimu.
Hajath Mastura akifurahia na wajukuu wake kile kinachoendelea #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
Muendelezo wa matukio ya picha #balazaLaIdd-Katoro #bukobawadau
#bukobawadau #balazaLaIdd-ItomaKatoro
Taswira muda mchache kabla ya shughuli kuanza rasmi
Sheikh Musthafa akiongoza Dua ya kuhitimisha shughuli ya maulid ya Baraza la Idd lililofanyika katika Viwanja vya Masjid Taawal uliopo Itoma Kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Ishara ya kuashiria Kukamilika kwa tukio la kihistoria Uzinduzi wa Mradi wa Maji Masjid Taawal Itoma-Katoro June 26,2017 kwa ufadhili mkubwa wa Bi Zahara Abdallah.
Furaha ikitawala mara baada ya maji kuanza kutiririka
Sehemu ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Katoro Islamic
Watoto wakuzaliwa na hajat Mastura Abdallah (103) wakicheck na Camera yetu
Upande wa Menu mambo yalikuwa safi pia
Wadau wakipata huduma ya chakula.
Kutoka maeneo ya Jikoni huduma ya mnuso ikiendelea..
Sheikh wa Mtaa wa Itoma akitoa neno na kuwakaribisha wageni mbalimbali walioweza kuhudhuria
Wanafamilia wakifurahia jambo kwa pamoja
Katika picha ni Bi Zahara na Mama yake mzazi hajat Mastura Abdallah (102.)