Bukobawadau

WABUNGE WA MKOA WA KAGERA WAKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA MJINI DODOMA LEO

Dodoma 9/06/2017.
Wabunge wa Mkoa wa Kagera wamefanya kikao na Mhe Balozi wa Uingereza Bi Sara Cooke kujadiliana juu ya misaada kwa maendeleo ya mkoa hususan ujenzi wa shule ya sekondari ya Ihungo iliyoharibika katika tetemeko la tarehe 10/09/2016. Serikali ya Uingereza inajenga shule hiyo upya kwa msaada wa Shs bilioni 6 uliotangazwa tarehe 2/01/2017 wakati. Bi Cooke alipokuwa mgeni rasmi wa mhe Rais John Pombe Magufuli alipotembelea mkoa wa Kagera kuwafariji wahanga wa tetemeko la tarehe 10/09/2016. Balozi huyo amethibitisha kwa Mwenyeji wake aliyemkaribisha katika kikao hicho Prof Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Kagera kwamba Uingereza pia itajenga nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya wasichana ya Rugambwa zilizoharibiwa na tetemeko. Itakumbukwa kwamba tarehe 2/01/2017 baada ya ziara ya Rais Profesa Tibaijuka alimsindikiza Balozi huyo akaione pia shule ya Rugambwa iliyoathirika kwa tetemeko. Juhudi hizo sasa zimezaa matunda.
Profesa Anna ni mmojawapo wa wasichana waliosoma shule ya Rugambwa ilipofunguliwa mwaka 1965. 

Wahe Prof Anna Tibaijuka (Muleba Kusini) Wilfred Lwakatare (Bukoba Manispaa) na Innocent Bashungwa (Karagwe) wapo katikati. Nd. Sylvester Ernest Afisa Mwandamizi wa Siasa Ubalozi wa Uingereza yu kulia.
Credit:Aidan Mapala
Next Post Previous Post
Bukobawadau