KATIKA KONGAMANO LA KIISLAMU LA AFRIKA MASHARIKI WILAYANI MULEBA LEO JULY 29,2017
Jamii
imetakiwa kuwatambua na kuwathamini wanawake kwenye ngazi mbalimbali kwa lengo
la kuwatumia kuepukana na matendo yanayoweza kuhatarisha usalama na matukio
yanayoangamiza dunia ya kuvunja amani
Wito huo
umetolewa leo hii Julai 29, 2017 na Sheikh Kassim Yusufu Husein kutoka Mombasa
nchini Kenya wakati akitoa mada ya thamani ya Mwananme kwenye kongamano la dini
ya kiislamu lililoandaliwa na Taasisi ya Ansary Muslimu iliyoko hapa
nchini ambalo limejumuisha masheikh
kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Sheikh Kassim
Yusufu Husein amesema wanawake wanayo majukumu makubwa katika kulea familia
hasa watoto wa jinsia zote lakini wamejaliwa na Mungu kulea hata waume zao
kiuadilifu iwapo mwanaume huyo naye atakuwa amelwlewa kwa misingi ya kiimani
katika matendo yanayokubaliwa na Mwenyezi Mungu
Amesema
katika kuwathamini wanawake hao wanatakiwa kuwa na sifa kadhaa mojawapo kuwa na elimu ya dini ya kiislamu kutambua miiko na mafundisho dini ikiwemo
ya elimu dunia kwa ajili ya kudhibiti matukio ya kuwanyima haki zao katika familia
na kwenye mazingira yanayomzunguka.
Amesema sifa
nyingine ni kuwa na hekima katika kuweka vitu mbalimbali kwa kila kimoja kuwa
katika mahali pake na hekima hiyo itamsaidia kuwalea watoto wake na mumewe na upatikanaji wake hutegemea
mazingira katika utoaji wa malezi.
Aidha Naibu
Mudil wa baraza la Wanasuna Tanzania (BASUTA) Sheikh Ally Zuberi kutoka mkoani
Tanga nchini Tanzania amewataka waumini
wa dini ya Kiislamu kuitafuta elimu kama alivyoamrishwa amtume Mohamadi SAW ili
kujihadhari na kubeba pipa laa moto siku ya Kiama baada ya kuondoka duniani
Kongamano hilo lililoanza jana Ijumaa
limehudhuriwa na masheik na waumini mbalimbali kutoka ndani na nje ya
Tanzania wakiwa pamoja wilayani Muleba mkoani Kagera huku baadhi yao wakifanya
biashara ya dawa za maradhi yanayomsibu mwanadamu, lakini kukiuzwa mavazi ya
kislamu kwa wqanaume na wanawake.
Mgeni rasmi
katika mihadhara ya kongamano hilo ni Sheikh Alif Nahad ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya The Islamic
Foundation Makao Makuu yaliyopo Mkoani Morogoro inayomiliki kituo cha TV ,
Radio Imaan na gazeti la Kiislamu la Imaan. Wanafunzi wa kiislamu wa Jakaya English medium school iliyoko muleba mjini wakiwa jukwaani kwenye kongamano hilo
Muonekan wa baadhi ya Wanafunzi wa kiislamu wa Jakaya English medium school iliyoko muleba mjini wakiwa jukwaani kwenye kongamano hilo
Picha zote Kwa hisani kubwa ya Mwanahabari wetu Shaaban Ndyamukama, MULEBA