Bukobawadau

MISA YA SHUKRANI YA MAREHEMU Sir GEORGE CLEMENT KAHAMA HUKO KAYANGA-KARANGWE



Matukio ya picha kutoka Kayanga Karagwe nyumbani kwa marehemu Sir George Kahama katika Misa ya Shukrani iliyoandaliwa na familia yake tarehe 19 July,2017.
Marehemu Sir George Clement Kahama pichani enzi za uhai wake.

Waumini wa Kikatoliki wakiwa wameungana na familia ya Marehemu Sir George Clement Kamaha katika Misa ya Shukrani iliyoongozwa na

KWANZA TUPATE HISTORIA FUPI YA BALOZI Sir GEORGE CLEMENT KAHAMA:
Balozi Clement George Kahama, aliyejulikana zaidi kama Sir George alizaliwa tarehe 30 Novemba, 1929 katika Wilaya ya Karagwe na kufariki dunia tarehe12 Marchi, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa Figo Renal Failure) kwa takribani miaka miwili.
Katika uhai wake, Marehemu alifanyakazi katika Serikali kwa vipindi mbalimbali zaidi ya miaka 50 ikiwemo awamu tatu za uongozi wa taifa hili baada ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961. Marehemu Sir George alikuwa miongoni mwa waafrika wachache waliopata fursa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria yaani Legislative Council mwaka 1957 na miaka miwili baadaye kuteuliwa kuwa Waziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito ya kikoloni kuelekea uhuru kwa nafasi ya Waziri wa Ushirika na Ustawi wa Maendeleo ya Jamii akiwa na Wenzake wazalendo Chief Abdalah Fundikira, Amir Jamal, na Solomon Eliufoo na Mwalimu akawa Waziri Kiongozi ( Chief Minister).

Baada ya Uhuru Mwaka 1961, Mhe Balozi George Kahama aliteuliwa kuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Baraza la Mawaziri la Watu tisa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru.Kutoka Uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2005 Sir George Kahama aliuteuliwa na Baba wa taifa na baadaye Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, kushika nyazifa za Wizara mbalimbali serikalini zikiwemo Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ushirika na Masoko, Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma na wakati huo huo akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).

Pichani ni Joseph na Anna George Kahama watoto wa Marehemu Sir George Clement Kahama

HISTORIA INAONYESHA :Katika muda wote wa utumishi wa Umma, Sir George aliaminiwa sana na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere baadaye Mhe Benjamin Mkapa kwa nyakati tofauti waliweza kumtuma katika nchi mbalimbali kuwa wakilisha kama mwakilishi maalum wa Rais (Special Envoy) katika nchi mbalimbali ikiwemo Zaire ambayo sasa inajulikana kama DRC, Burundi na Rwanda, Holy See (Vatican) na nchi nyingine.

Pichani Mzee Pius Ngeze na mke wake wakiwa katika misa ya Shukrani ya Marehemu Sir George Clement Kahama iliyofanyika nyumbani kwake Kayanga Karagwe.

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiongoza Misa ya Shukrani ya Marehemu Sir Clement George Kahama

Kazi nyingine alizowahi kufanya Mhe Sir George Kahama ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Maendeleo la taifa (NDC),taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia uanzishwaji wa Viwanda nchini, Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Kituo cha Kuvutia wawekezaji (IPC) ambacho baadaye kimekuja kujulikana kama Tanzania Investment Centre-TIC. Kablaya Uhuru Sir George alikuwa kiongozi wa Chama cha ushirika cha Bukoba, chama ambacho kilitoa msaada mkubwa wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi na kuimarisha TANU kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya Ushirika katika maenembalimbal nchini. Itakumbukwa kuwa Wazalendo watano waliounda Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito mwaka 1959 akiwemo Mzee Paul Bomani, Chief Abdullah Fundikira (Tabora), Solmon Eliufoo (Kilimanjaro), Amir Jamal ( Morogoro) na Kahama Mwenyewe (Kagera) walikuwa viongozi katika vyama vya ushirika katika maeneo waliyotoka

Adv.Protas Ishengoma pichani kushoto akiwa amejumuika na waumini wengine kushiriki Misa hiyo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kijijini Kayanga Karagwe.

Aidha, katika Uhai wake, Sir George Kahama aliwahi kutumikia taifa katika nyanja za kidiplomasia kama Balozi wa Tanzania Ujerumani mwaka 1965-1966, Baloziwa Tanzania China (1984- 1989) na Balozi wa Tanzania Zimbabwe (1989-1991).
Katika uhai wake, Sir George Kahama aliwahi kutunikiwa nishani mbalimbali za kitaifa na Kimataifaikiwemo Knight Commander of the Order of St. Gregory the Great iliyotolewana Pope John XXIIImwaka 1962. Hii ndiyo nishaniiliyozaajina la Sir George.Nishani zingineni kama“The Order of Kilimanjaro iliyotolewa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi 1990, ambayo ni nishani ya juu kabisa wanayotunukiwa watumishi wa umma.

Mwaka 1975-1976 alikuwa Mjumbe wa Kundi la Watu Mashuhuri duniani walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya utafiti kuhusu athari za Uendeshaji wa Makampuni Makubwa ya Kimataifa katika uchumi wa nchi zanazoendelea.

Mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Chama cha Mapinduzi na Serikali ikiwemo Serikali kuhamia Dodoma kwa kasi kubwa na chama kuimarika zaidi kumetokea siku chache kabla ya kufariki kwake na kutimiza ndoto yake zaidi ya miaka 40 aliyojishughulisha na mradi wa Ustawishaji ya Makao Makuu.

Mwaka 197;Sir George aliteuliwa na Serikali ya Nigeria kama Mjumbe wa Kamati ya watu watatu waliopewa kazi ya kufanya tathmini ya mchakato wa uhamishaji wa Mji Mkuuwa Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja.

Sir George aliwahi kuandika maandiko na vitabu mbalimbali katika Nyanja za Kidiplomasia,Ushirika,Uchumi,Maendeleo ya Ujenzi,ikiwemo kitabu cha “The Challenge for Tanzania’s Economy” kilichochapishwa na kampuni ya JamesCurrey Heinemann ya Uingelezana “Tanzania into the 21stCentury”,pia alichangia kuandika kitabu cha “The First Tanganyika Industrial Development Blue Print” pamoja na Arthur D. Little Inc. wa Marekani.

Mbali na utumishi Serikalini Sir George Kahama alikuwa Baba mzuri wa familia aliyependa umoja wa familia na alikuwa baba tuliyemtegemea kwa ushauri na dira katika maishayetu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe!!

Baadhi ya waumini kutoka maeneo mbalimbali walioweza kuhudhuria Misa hiyo

Kutoka kushoto ni Askofu Almachius Vincent Rweyengoza wa jimbo katoliki ya Kayanga wakati Ibada inaendelea..

Wakati wa kutoa vipawa.

Utaratibu wa Waumini kutoa vipao vyao

Shughuli nzima iliongozwa na Bwana Rwazo pichani kulia kama anavyo onekana akipokea maelekezo kutoka kwa Anna ambaye ni Binti wa Marehemu Sir George Clement Kahama.

Familia ilifanya utaratibu wa kusafirisha Udongo baada ya kuzingatia msimamo wa Marehemu uliowalazimu kufanya mazishi yake Jijini Dar Es Salaam katika makaburi ya Kinondoni mnano tarehe 16 machi,2017


Tukio linaloendelea katika picha ni wakupeleka udongo kwenye kaburi.

Askofu Rweyongeza ndiye aliyeongoza utaratibu wa kuweka Udongo kwenye kaburi lililopo mbele ya nyumba ya marehemu Sir George Clement Kahama


Bukobawadau media tunatoa pole kwa wafiwa wote

Muonekano wa Kaburi lililowekwa Udongo kama Ishara ya kukamilisha taratibu za kimila za kumzika mtu nyumbani kwao,Apumzike kwa Amani mpendwa wetu Sir George Kahama

Ni simanzi na huzuni mkubwa kwa Mama Kahama mara baada ya tukio la kuweka Udongo,kushoto pichani anaonekana Mama Luangisa akimfariji.

Tukio jingine na kihistoria lililofuata ni kumsimika Mkuu wa familia ya Marehemu Sir George Kahama, tukio lililongozwa na Viongozi wa Kimila wa Ukoo na kufatia na baraka kutoka kwa Baba Askofu Kilaini

Askofu Almachius Vincent Rweyengoza wa jimbo katoliki ya Kayanga akitoa neno mara baada ya kusimikwa kwa Mkuu wa familia nafasi aliyopewa mtoto mkubwa wa Marehemu Bw. Joseph Kahama pichani kulia.

Pichani kushoto ni Mrs Joseph Kahama akifatilia kwa umakini tukio la kihistoria la kumsimika mme wake kama mkuu wa familia (Mulangira)

Bwana Kwame Luangisa akibadilishana mawazo na Bi Tunu Mwapachu.

Kiongozi wa Ukoo akiendelea na taratibu za kimila za kumsimka Bwana Joseph Kahama kama mkuu wa familia , tukio lililofanyika mara baada ya Misa maalum ya Shukrani

Kushoto ni Mzee Masabala na kulia kwake ni Adv. Protas Ishengoma marafiki wa familia.

Sasa ni Mulangira Joseph Kahama  (Ta' Joseph) mara baada ya kusimikwa rasmi na kukabiziwaa Mkuki ,dhana ya kimila na kutambuliwa kama mkuu wa familia

Mama Mzazi wakati akimpongeza mwanae kwa kusimikwa kuwa msimamizi mkuu wa familia ya Marehemu Sir George Clement Kahama.

Bwana Joseph Kahama anapokea pongezi kufuatia tukio hilo la kihistoria
















Anapongezwa na Mama Luangisa pichani kushoto

Pongezi kutoka kwa mama wadogo



Neno kutoka kwa Joseph Kahama kwa niaba yake na kwa niaba ya familia ambapo ametumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kabisa kwa viongozi wote wa nchi kuanzia hawamu ya pili mpaka hawamu ya tano kufuatia ushirikiano mkubwa waliohupata toka kipindi cha kumuuguza Mzazi wao mpaka mauti yalipo mkuta

Watoto wa Marehemu Mzee Samuel Luangisa wakati wa utambulisho,Marehemu Mzee Samuel Luangisa alikuwa rafiki wa wengi,mshauri,mwalimu na mwanadiplomasia wa kweli.Aliipenda na kuicheza siasa tangu ujana wake MPAKA kipenga cha mwisho,Uvumilivu na uchangamfu wake ulimfanya kukubalika kwa kila rika,alitetea kile alichokiamini kwa kuzipanga vizuri karata zake.


Mzee Lutabingwa pichani kulia mmoja wa marafiki wakubwa wa familia ya Marehemu Sir George Clement Kahama aliyezaliwa Nov 30,1929 na kufariki Tarehe 12 Machi,2017.


Dk Kabakama wakati wa utambulisho

Chief Edward Makwahia kutoka Shinyanga akiwapungia watu mikono wakati wa Utambulisho

Mzee Rwechungura Isaack akitoa Salaam

Sehemu ya wanakwaya mara baada ya kuwajibika

Kushoto ni Meneja wa CRDB Bank Tawi la Kayanga Karagwe

Sehemu ya waalikwa ukumbini

Chief Edward Makwahia wa Usukumani akitoa neno

Adv. Protas Ishengoma akitoa neno kama rafiki na mtunza Siri aliyeaminiwa na Marehemu Sir George Clement Kahama

Kiongozi wa Ulinzi Kata Kayanga akitoa neno

Kati ya Wageni mashuhuli walioweza kuhudhuria ni pamoja na Mama Kabaka wa Uganda pichani kushoto.

Al hajji Omary Kyamani mkazi wa Karagwe.

Mzee Bitegeleize mdau wa Maendeleo Wilayani Karagwe

Umati mkubwa wa watu wameweza kushiriki Shughuli hiyo iliyofanyika juma lililopita nyumbani kwa marehemu Sir George Kaham

Muendelezo wa Salaam za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali

Salaam za pongezi na nasaha zikitolewa kwa Joseph Kahama kufuatia tukio la kusimikwa kama Mkuu wa familia hiyo


Bwana Uhuru Luangisa pichani kulia akifatilia kinachojiri

Mbunge Lwaatare akitoa neno

Mama wa familia akitoa neno na Shukrani zake kwa watu wote walioweza kuhudhuria shughuli hiyo


Kamati ya Maandalizi ya Shughuli nzima ikitoa utambulisho


Baba Askofu Kilaini akisalimiana na Adv Protas Ishengoma pichani kulia

Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli hiyo



Waalikwa wakibadilishana mawazo na Mama Kahama mara baada ya shughuli kukamilika

Picha kwa ajili ya kumbukumbu

Bi Tunu Mwapachu katika picha ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo na Mama Kahama.

Taswira mbalimbali ukumbini shughuli ikiendelea

Baadhi ya waalikwa wakiagana na wanafamilia

Bi Rose Luangisa na mwanae akiwa ameongozana na mme wake muda mchache kabla ya Safari yao ya kurejea Mjini Bukoba kutoka eneo la tukio Kijijini Kayanga Karagwe.


Menu husika ikiwa tayari mezani


Waalikwa wakiendelea kupata huduma safi ya chakula kilichoandaliwa

Sasa ni mwendo wa Burudani.

Bi Rose Luangisa akisaini kitabu cha kumbukumbu katika Misa maalum ya Marehemu Sir George Clement Kahama.

Utaratibu wa kusaini katika kitabu cha kumbukumbu kilichoandaliwa na familia ukiendelea

Askofu Almachius Vincent Rweyengoza wa jimbo katoliki ya Kayanga akisaini kitabu cha kumbukumbu katika Misa maalum ya Marehemu Sir George Clement Kahama.

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare akisaini katika kitabu cha kumbukumbu katika Misa ya Shukrani ya Marehemu Sir George Kahama

Bi Anna Luangisa na Kijana David wakicheck na Camera yetu moja kwa moja kutoka eneo la tukio Kayanga Karagwe

Muonekano wa barabara kati ya Kayanga na Omurushaka Karagwe.

Muonekano wa barabara ya Kayanga -Omulushaka

BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043
Instagram @bukobawadau
Binti Luangisa pichani hakika tumkumbuke Mzee wetu kwa yale mema yote aliyoyafanya!!
Mdau Christhopher Chichi pichani
Kama Kristo alivyokufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Kristu Mungu atawaleta pamoja nao
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe!!








Next Post Previous Post
Bukobawadau