MZEE GOTFRIED RWELA MKAZI WA KARAGWE ASHEREKEA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWAKE!
Mkazi wa Kijiji cha Kinyinya, wilayani Karagwe mkoani Kagera, Gotfried
Rwela akikata keki wakati akisherehekea kutimiza umri wa miaka 100 ,
katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, jana. Gotfried amezaliwa
mwaka 1917 ana wake wawili, watoto 18, wajukuu 49 na vitukuu 19.
Mzee Gotfried Rwela akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake wa kuwazaa.
Pichani wapo wanafamilia na baadhi ya wazee waliobahatika kusima na Mzee Gotfried Rwela
Pichani ni Vitukuu wa Mzee Gotfried Rwela wakati wa utambulisho
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika sherehe hiyo
Picha zote kwa hisani ya Shaaban Ndyamukama
Pongezi zikiendelea kutoka kwa wazee mbalimbali aliosoma nao na kufanya nao Kazi akiwemo Askofu Mstaafu ya ELCT Dayosisi ya Kagera
KARAGWE:Jamii imetakiwa kuwalea watoto na mama zao kwa kuzingatia
misingi ya imani zao za kiroho katika kufundisha maadili mema na
kuwafanya watoto hao kuwa na tabia njema ya kuthaminiana baina yao na walezi
wanaowazunguka.
Wito huo umetolewa na mzee mmoja mkazi wa kitongoji
cha Kinyinya katika kijiji cha Kituntu
wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Mzee Gotfried Ruyumbu Rwela ambaye alikuwa
akifanya sherehe ya kufikisha miaka 100
ya kuzaliwa wilayani humo na kwamba upendo
na maadili vimemsaidia kuishi maisha marefu
Mzee Rwela amesema katika kufanya kazi za kijamii
watumishi wa sekta mbalimbali wanatakiwa
kutanguliza uaminifu ,utiifu na ubunifu kwa kuhakikisha yanapatikana maendeleo kwa kila mmoja kutimiza wajibu
na majukumu yake.
Aidha mzee huyo alizaliwa mwaka 1917 na kuanza shule
mwaka 1935 kisha kuanza kazi ya ualimu wa shule za msingi mwaka 1952 amejaliwa
kuwa na wanawake wawili na watoto
18, wajukuu 49 na vitukuu 19
Katika utumishi wake kama mwalimu alifundisha
wanafunzi wengi akianzia mkoani Shinyanga mwaka 1962 na amestaafu mwaka
1982 akiwa wilayani Karagwe ambaye
amedai kwamba katika mfumo wa maisha ya
familia msingi mkubwa ni upendo, nidhamu na kuunganisha umoja kwa watoto jinsia
zote
Baadhi ya viongozi na watu wa
rika tofauti wakiwemo watoto wake,
wajukuu na vitukuu wamempongeza mzee huyo kufikisha umri wa miaka 100 ya
kuzaliwa wakimuombea maisha marefu kuendeleza hekima, upendo na malezi ya kirohoMzee Gotfried Rwela akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake wa kuwazaa.
Pichani wapo wanafamilia na baadhi ya wazee waliobahatika kusima na Mzee Gotfried Rwela
Pichani ni Vitukuu wa Mzee Gotfried Rwela wakati wa utambulisho
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika sherehe hiyo
Picha zote kwa hisani ya Shaaban Ndyamukama
Pongezi zikiendelea kutoka kwa wazee mbalimbali aliosoma nao na kufanya nao Kazi akiwemo Askofu Mstaafu ya ELCT Dayosisi ya Kagera