Bukobawadau

WASHABIKI WA MUZIKI NCHINI WAZISUBIRI KOLABO MATATA ZA COKE STUDIO KWA SHAUKU

Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni
Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi
Baadhi ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.
---
Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje, washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba na kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria Kimani na 2Face.
Katika msimu wa Coke Studio wasanii wanaoshiriki wanatokea katika nchi za Kenya,Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon wakisindikizwa na mwanamuziki nguli wa kimataifa kutoka nchini Marekani Jason Derulo.
Mbali na wasanii kutoka Tanzania wakali wengine wa muziki kutoka nchi za Afrika wanaoshiriki msimu huu ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).
Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic,Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana
Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola ambayo iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika na kuzidi kuifanya Afrika izungumze lugha moja tu ya muziki.
Imelielezea zaidi kuwa onyesho hilo kuwa lina lengo la kukusanya pamoja wasanii na kuonyesha uwezo na vipaji vya muziki vilivyopo Afrika ikiwemo kutoa fursa kwa wasanii chipukizi kufanya kazi na baadhi ya wasanii na watayarishaji wa muziki wa kimataifa,vilevile Kuwakusanya wasanii wanaofanya aina tofauti ya muziki, wanaotoka katika nchi tofauti za Kiafrika kuwawezesha kutengeneza sauti ya Afrika kupitia burudani ya muziki
Coca Cola Coke Studio pia inaleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
Next Post Previous Post
Bukobawadau