KANISA LATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU BIHARAMULO
Kanisa la FPTC linalotoa huduma za kiroho katika wilaya ya
Biharamulo mkoani Kagera kwa kushirikiana na wafadhili kutoka nchini
Finland limetoa msaaa wa baiskeli 24 na kilo 200 za mahindi kwa watoto 30
wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo kwa gharama ya Sh10.88
milioni
Akikabidhi msaada huo jana Mratibu wa mradi wa kuhudumia
walemavu katika kanisa hilo Lizia Masele alisema watoto hao wenye
mahitaji maalum wapata Baiskeli 10 za kawaida , Wheelchair 10, Trycycle nne na
blocks seti mbili kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi
Kabindi na Biharamulo mjini.
Masele alisema kanisa hilo kwa kushirikiana na wafadhili wa Finland
wanafanya kazi ya kutoe elimu kwa jamii kuhimiza haki za watoto, kusaidia
watoto wenye ulemavu kupata elimu, kuwanunulia vifaa watoto wenye mahitaji
maalum na kuwatibisha walemavu wenye kuwa na maradhi yanayotibika.
“Shughuli zetu tunashirikiana na mfadhili Maria Holmberg kutoka Finland
ambaye ni mshauri wetu lakini tukishauriana na watendaji mbalimbali katika
ofisi ya mkurugenzi wa wilaya hii na kupata ufanisi mkubwa” Alisema
MaselePichani kushoto Diwani wa Kata Nyamahanga Amon Movati na Afisa tarafa ya Nyarubungo wilayani Biharamulo mkoani Kagera Nyambuli Siangi (pichani kulia) wakitoa msaada kwa watoto wenye ulemavu
Afisa ustawi wa Jamii Ladislaus Raulent na Afisa tarafa ya Nyarubungo Nyambuli Siangi, waliomba wafadhili hao kuendelea kusaidia watu wenye ulemavu wakati serikali ikitafuta fedha za kuboresha mazingira yanayowazunguka, hasa katika shule zenye wanafunzi wenye ulemavu na sehemu za kazi kwa watu wazima.
Pia Afisa ustawi wa jamii
aliwashauri baadhi ya wazazi au walezi kutumia rasilimali zinazowazunguka
kuwapatia chakula chenye lishe watoto wao hata kama wanakabiliwa na
ulemavu waweze kukua kiafya badala ya kupatwa na utapiamlo
unaodhoofisha afya zao.
Hata hivyo mfadhili wa kanisa hilo na watoto wenye mahitaji maalum
kutoka Finland Maria Holmberg alisema nchi yake imepunguza utoaji misaada kwa
kanisa hilo kwa sababu ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo
kanisa haliwafikii walengwa kwa kukosa usafiri wa kuwafikia kutokana na ubovu
wa barabara vijijiniMaria Holmberg kutoka nchini Finland (mzungu) akiwakabidhi baiskeli za aina mbalimbali watoto wenye ulemavu wakiwa na wazazi wao katika kanisa la FPTC lililopo kata ya Nyamahanga wilayani Biharamulo mkoani Kagera
Maria Holmberg kutoka nchini Finland akiwakabidhi baiskeli za aina mbalimbali watoto wenye ulemavu wakiwa na wazazi wao katika kanisa la FPTC lililopo kata ya Nyamahanga wilayani Biharamulo mkoani Kagera
Picha na Shaaban Ndyamukama