Bukobawadau

HABARI PICHA SHUGHULI YA MATANGA YA MAMA ESTHER RWEGASIRA HUKO KIJIJINI KANYIGO

Baadhi ya watoto wa familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Marehemu Balozi Joseph Rwegasira wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Ibada maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Mama yao Mzazi Mareheme Mama Esther Rwegasira ibada iliyofanyika Mwishoni mwa juma Nyumbani kwake Kijijini Kanyigo Bukoba.
Watoto wa Marehemu mzee Joseph Rwegasira na Mama Esther Rwegasira pichani hii
Bi Joanitha Rwegasira (Mrs Shuli)
Mjukuu wa Mama Esther Rwegasira akiwa kwenye kaburi la Marehemu Bibi yake Mpendwa.
Anaonekana Bw. Lutta mtoto wa mwisho wa Marehemu Bi Esther Rwegasira katika picha ya kumbukumbu kwenye kaburi la Marehemu Mama yake Mpendwa.
Muonekano wa Kaburi la Marehemu Balozi Joseph Rwegasira aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje,na Mbunge wa Nkenge mpaka mwaka 2000
Paroko akiongoza Ibada ya shukrani na kumaliza matanga Mwaka Mmoja kifo cha Mama Esther Rwegasira
Sehemu ya waumini wakiendelea kushiriki Ibada ya shukrani na kumaliza matanga Mwaka Mmoja kifo cha Mama Esther Rwegasira
Ibada ya shukrani na kumaliza matanga Mwaka Mmoja kifo cha Mama Esther Rwegasira ikiwa enaendelea nyumbani kwake Kijijini Bugombe Kanyigo siku ya Jumamosi Aug 26,2017
Shughuli ya Ibada ikiwa inaendelea.
Pichani ni makundi mbalimbali ya watu walioweza kushiriki Ibada hiyo iliyofanyika Siku ya Jumamosi Aug 26,2017 Nyumbani kwa familia ya Marehemu Balozi Joseph Rwegasira
Pichani kulia ni Dr. Mboneko rafiki wa karibu wa familia ya Marehemu Mama Esther na Balozi Rwegasira,Wapumzike kwa amani!
Familia ya Bw Julius (Tiba) Rwegasira pichani
Paroko wa kanisa katoliki Mugana akiendelea kuongoza Ibada ya kumbukumbu na kumaliza Matanga mwaka mmoja kifo cha marehemu Mama Esther Rwegasira
 Shughuli ya Ibada ya  kumbukumbu na kumaliza Matanga mwaka mmoja kifo cha marehemu Mama Esther Rwegasira ikiwa inaendelea
Pichani ni makundi mbalimbali ya watu walioweza kushiriki Ibada hiyo iliyofanyika Siku ya Jumamosi Aug 26,2017 Nyumbani kwa familia ya Marehemu Balozi Joseph Rwegasira
Bi Joanitha Rwegasira wakati Ibada maalum ya kuwaombea wazazi wake ikiendelea.
Bwana Tiba na mke wake Edith wakiendelea kushiriki Ibada ya kumbukumbu mwaka mmoja kifo cha mama yao mpendwa Marehemu Esther Rwegasira.
Mamia ya watu wakiendelea kushiriki shughuli ya Ibada ya Kumbukumbu mwaka mmoja kifo cha Marehemu Bi Esther Rwegasira
Wanakwaya wakiendelea kuwajiba kwa nyimbo cha mapambio
Muda wa kutoa Sadaka.
Sehemu ya waumini katika utayari wa kutoa sadaka zao
Utaratibu wa kutoa Sadaka ukiendelea kwa watu wote
Mwana wa Kanyigo akishow love mbele ya Camera yetu
 Mzee Henry Muyanga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia ya arehemu Mzee Rwegasira
Mdau kutoka familia ya Marehemu Dominic Mgomba akiendelea kushiriki shughuli hiyo
Huu ni muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli ya kumaliza Matanga (mwaka mmoja) Kifo cha mpendwa wetu Bi Esther Rwegasira aliyekuwa Mke wa Marehemu Balozi Joseph Rwegasira aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara serikali ya awamu ya pili
Wakati wa utambulisho kwa wanafamilia
Katikati ni Bi Doris Mwansasu binti wa Marehemu Mama Esther Rwegasira
Wapili kutoka kulia pichani ni Bi Pamella binti wa Marehemu Mama Esther Rwegasira
Watoto wa familia ya Marehemu Mama Esther Rwegasira wakati wa Utambulisho
Mtoto mkubwa wa kuzaliwa na Marehemu Mama Esther Rwegasira,Julius (Tiba) Rwegasira akitoa neno la shukrani kwa watu wote waliohudhuria shughuli ya Ibada maalum ya kumaliza msiba mwaka mmoja kifo cha mama yao mpendwa.
Ni simanzi kubwa na vilio kwa watu wote wakati wa utambulisho na neno la shukrani kutoka kwa watoto wa Marehemu Bi Esther Rwegasira.
Machozi ya huzini yakiwatoka kufuatia maneno ya simanzi yaliyotolewa na watoto wa Marehemu Mama Esther Rwegasira.
 Wakati Bi Juanitha Rwegasira akitoa neno la shukrani kwa watu wote waliohudhuria Ibada hiyo iliyofanyika nyumbani kwao kijijini Bugombe Kanyigo Wilayani Missenyi.
 Vilio na machozi yakiwatoka wananchi kufuatia maneno ya Bi Joanitha Rwegasira
Maswala ya Selfie yakiendelea kuchukua kasi..!
Pata mtiririko wa matukio ya picha kutoka eneo la kaburi la Marehemu mama yetu Mpendwa Esther Rwegasira


Muendelezo wa matukio ya picha kumbukumbu ya  mwaka mmoja kifo cha Bi Esther Rwegasira
Wanafamilia wakishiriki kuweka maua na Mashada kwenye Kaburi la Marehemu Mama Esther Rwegasira
Ibada maalum ikiendelea Katika Kaburi la Mama Esther Rwegasira mke wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1993 hadi 1995, Balozi Joseph Rwegasira
Bi Edith Rwegasira (Mrs Tiba) akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Balozi Joseph Rwegasira
Padre akiongoza Sala kwenye kaburi la Marehemu Mzee Rwegasira.
Taswira mbalimbali wanafamilia wakiwa tayari kwa ajili ya kuweka maua na mashada kwenye kaburi la Marehemu Balozi Joseph Rwegasira.
Kaburi la Marehemu Balozi Joseph Clemence Rwegasira
Muendelezo wa matukio ya picha kumbukumbu ya mwaka mmoja kifo cha Marehemu Bi Esther Rwegasira
Bi Joanitha akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yake mzazi


Huu ni muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli ya kumaliza Matanga (mwaka mmoja) Kifo cha mpendwa wetu Bi Esther Rwegasira aliyekuwa Mke wa Marehemu Balozi Joseph Rwegasira aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara,
Muendelezo wa matukio ya picha eneo la kaburi wakati wanafamilia wakiweka mashada ya maua na mishumaa.
Hakika ni simanzi kubwa
Bwana Edgar Osward rafiki wa familia ya marehemu Balozi Joseph Rwegasira
 Huduma safi ya Msosi ilitolewa na Mwanamama mpambanaji maarufu kwa jina la Mama Mussa pichani



 Mtu na shemeji yake pichani
 Katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu Bi Joanitha na mme wake Mr Shuli.
Mdau Lutta Rwegasira pichani
Matukio ya picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu kupitia Bukobawadau Media.
Muendelezo wa matukio ya picha kwa wanafamilia kwa ajili ya kumbukumbu kulia kabisa ni Bi Pamella binti ya Marehemu Esther Rwegasira
 Bwana Gwakisa na Mke wake katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu kwenye kaburi la Marehemu Balozi Joseph Rwegasira
Sehemu ya wadau pichani wakiwa tayari kwa ajili ya kupata huduma ya Chakula
Wadau wakiendelea kupata msosi




Taswira mbalimbali wakati huduma ya chakula ikiendelea kutolewa
 Taswira mbalimbali eneo la tukio wakati huduma ya Chakula ikiendelea kutolewa Sawa bin haki kwa watu wote
Muonekano wa kitu Menu katika shughuli hiyo iliyofanyika Jumamosi Aug 26,2017 Kijijini Kanyigo
 Nyota wa siku ni Mzee Balitemao Tibawa kikongwe anayesemekana kuwa na umri wa Miaka 106 na afya yake bado imeimarika,anaonekana mwenye nguvu nakuweza kushiriki matukio ya kijamii ni Mkazi wa Kijiji Bukombe Kanyigo Wilayani Missenyi
BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043
Mwisho Taswira Kijijini Bugombe Kanyigo kupitia Bukobawadau Media

Next Post Previous Post
Bukobawadau