Bukobawadau

MKUU WA MKOA WA KAGERA ATOA MAAGIZO MAKALI KWA WANANCHI NA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOENDELEA KUKAIDI MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu wa Pili Kutoka Kulia Akisikiliza Maelezo Kutoka kwa Mhifadhi wa Msitu wa Biharamulo Mrefu Kuliko Wote
  Baadhi ya Eneo la Msitu wa Biharamulo Lililoharibiwa Kwa Kuchoma Mkaa
 Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Kijuu Akiongea na Wananchi wa Nemba Biharamulo
 Mkuu wa Mkoa na Msafara Wake Wakiangalia Eneo Lililozibwa na Mwananchi na Kuzuia maji kutiririka kufuata Mkondo wakae katika Msitu wa Nyantakara Karibu na Kijiji Mpago
 Huyo ndiye anajiita Balozi wa wananchi walioanzisha makazi katikati ya Msitu Nyantakala makazi yanyoitwa MOBASA RAHA​
 Eneo Hili Mwananchi anachimba mtaro kuizuia maji yasifuate mkondo wake Mkuu wa Mkoa Kijuu aliagiza eneo hilo kurekebishwa na kurudia katia hali ya ya zamani mara moja

Na: Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu afanya ziara katika Misitu ya Hifadhi ya Biharamulo na Nyantakala Wilayani Biharamulo kuona kama agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wavamizi wa misitu hiyo kuondoka mara moja alilolitoa tarehe 19 Julai, 2017 alipofanya ziara yake Mkoani Kagera.
Rais Magufuli akiwa Wilayani Biharamulo Julai 19, 2017 aliagiza wavamizi wote wa Misitu ya Asili na Wafugaji waliovamia Mapori ya Akiba kuhakikisha wanaondoka mara moja katika hifadhi na watakaokaidi wachukuliwe hatua za kisheria.
Hatua hiyo ilitokana na operesheni ondoa mifugo iliyofanyika Mkoani kagera kunusuru Misitu ya asili, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambavyo vilikuwa vimevamiwa na kuharibiwa kwa kiwango kikubwa kwa kukata mkaa, kuendesha kilimo na kuingiza mifugo katika Misitu na Mapori ya Akiba.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu akitembelea Misitu ya Biharamulo na Nyantakala Wilaya Biharamulo Agosti 22, 2017 bado alikuta shughuli za uharibifu wa uchomaji wa mkaa katika misitu hiyo ukiwa unaendelea kwa baadhi ya wananchi wachache, pia waliokaidi kuondoka katika makazi waliyoyaanzisha katika Misitu hiyo jambo ambalo lilipelekea atoe maagizo makali kama ifuatavyo;
Mkuu wa Mkoa Kijuu alimwagiza Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kufikia tarehe 26 Agosti, 2017 awe amesitisha mara moja vibali vyote vya umiliki na uvunaji wa miti kwenye mashamba ambayo yanamilikiwa na wananchi yaliyopo jirani na Hifadhi za Misitu ya Biharamulo na Nyantakala kwa kuwa wamiliki hao wanayatumia mashamba hayo ya miti kama ngao huku wakifanya uhribifu wa uchomaji mkaa katika misitu hifadhi.
Agizo la pili, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpago Bw. Yasin Mahanga asimamie uvunjwaji wa matuta yanayozuia maji kupita katika mkondo wake kwenye bonde la msitu Nyantakala pia kuwaondoa wananchi wote wanaoendesha kilimo katika bonde hilo mara moja na kumzuia mwananchi anayewatoza fedha wafugaji kunywesha maji mifugo yao katika lambo lililopo katika bonde hilo kuacha tabia hiyo mara moja vinginevyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Agizo la tatu la Mkuu wa Mkoa Kijuu ni kwa wananchi waliovamia na kuanzisha makazi katika Msitu wa Nyantakala na kuyabatiza makazi hayo jina la MOMBASA RAHA kuondoka mara moja ifikapo tarehe 9 Septemba, 2017. Wasipoondoka wenyewe hadi tarehe 10 Septemba, 2017 Mhe. Kijuu ameagiza Jeshi la Polisi kuvunja makazi hayo na kuwalazimisha wananchi wavamizi kuondoka kwa lazima.
Mhe. Kijuu anaendelea na ziara ya katika Mapori ya Akiba ya Burigi na Kasindaga kujionea mwenyewe kama agizo la Rais John Pombe Magufuli limezingatiwa na kutekelezwa kikamilifu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau