Bukobawadau

SERIKALI MKOANI KAGERA YAPOKEA VIFAA VYA AFYA VYENYE THAMANI YA MILIONI KUMI KUTOKA MPANGO WA USAID BORESHA AFYA

Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
 Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
 Picha ya Pamoja Mara baada ya Vifaa Kukabidhiwa


Serikali Mkoani Kagera yapokea vifaa vya Afya vyenye thamani ya shilingi Milioni Kumi kutoka kwa wadau wa maendeleo wa mpango wa USAID Boresha Afya ambao ni wadau muhimu katika Sekta ya Afya kwa Mkoa wa Kagera.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Meneja wa mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera Bw.Charles Kato katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Agosti 21, 2017 ambapo vilipokelwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu.
Akikabidhi vifaa hivyo Bw. Kato alisema ni mahsusi kwa kituo cha Afya Kabyaile ambacho kimejengwa upya na Serikali baada ya kile cha awali kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi mwaka jana Septemba 10, 2017.
Aidha, Dk. Kato alisema kuwa vifaa vimetolewa na Mpango wa USAID Boresha Afya ambao unatekelezwa katika Wilaya ya zote za Mkoa wa Kagera. “Mpango huu wenye malengo ya kuchangia juhudi za Serikali za kuboresha Afya ya Mama na mtoto  unafadhiliwa na USAID na PATH pamoja na Serikali.” Alifafanua Bw. Kato
Pia Bw. Kato alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo la kuchangia mikakati ya Serikali ya kuhakikisha kituo kipya cha Kabyaile kinatoa huduma bora hasa kwa wakina mama na watoto.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwashukuru wadau hao waliotoa vifaa hivyo na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuboresha huduma za wananchi hasa wakina mama na watoto katika Mkoa wa Kagera.
Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo alikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila ambaye naye alitoa shukrani za Wilaya yake kwa USAID Boresha Afya  kuwa wamekuwa wadau wapili kutoa msaada wao katika Kituo cha Kabyaile baada ya Benki ya NMB nao kutoa msaada wao na kutoa wito kwa wadau wngine kujitolea.
Vifaa vilivyotolewa ni Seti moja ya vifaa vya upasuaji wakati wa kujifungua, Seti moja ya vifaa vya kuzalisha, Mashine moja ya utakasaji wa vifaa, Seti mbili za kumsaidia mtoto kupumulia na kitanda kimo cha kujifungulia.
Next Post Previous Post
Bukobawadau