DOKTA MPANGO AIHIMIZA WAINGEREZA KUKUZA ZAIDI BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto), akiongoza majadiliano
na Ujumbe wa Wabunge watano pamoja na maafisa kadhaa kutoka nchini Uingereza,
walipomtembela na kufanya naye mazungumzo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wabunge wa mabunge ya Uingereza wakiwa katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt, Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungungumzo na wabunge kutoka nchini Uingereza waliomtembelea Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba.
Baadhi ya Ujumbe kutoka Tanzania walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na baadhi ya Wabunge kutoka nchini Uingereza, Jijini Dar es Salaam (kulia ni Mkurugenzi wa masuala ya Sheria Bi. Susana Mkapa akifuatiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Paul Sangawe.
Kamisha wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Mgonya Benedicto (kushoto) na Msajili wa Hazina, Dkt. Oswald Mashindano, wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na wageni wake, Wabunge wa Mabunge ya Uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi).
Kiongozi wa Wabunge wa Bunge la Uingereza waliotembelea nchini na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mhe. David Linden, akizungumza namna nchi hiyo inavyosaidia masuala mbalimbali
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akizungumza na Wabunge kutoka Nchini Uingereza waliomtembelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na kuipongeza nchi hiyo kwa kuisadia Tanzania katika masuala mbalimbali, amesisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili ujikite zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Uingereza, Mhe. David Linden (katikati) na Wabunge wengine kutoka Uingereza, Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Mwisho

Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati)akijadili jambo na baadhi
ya maafisa walioambatana na Wabunge wa Bunge la Uingereza baada ya kumalizika
kwa Mkutano kati yao ulioangazia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano, Elimu, lishe, na Matumizi adili ya rasilimali fedha, Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Tanzania
imetoa rai kwa Serikali ya Uingereza kubadili mfumo wa uhusiano wake
kwa kujikita zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji badala ya
kutoa misaada ya kawaida ili nchi iweze kukuza uchumi wake kwa haraka
zaidi.
Wito
huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Isdor Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa
wabunge kutoka mabunge ya uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la
Wawakilishi).
Dokta
Mpango amesema kuwa kiwango cha mtaji ambacho Serikali ya Uingereza
imewekeza nchini hadi sasa ni Paundi bilioni 2.5 lakini kwa upande wa
biashara kati ya nchi hizo mbili, hali si nzuri.
"Mwaka
2015 Tanzania iliuza nje bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 22.5 na kununua bidhaa kutoka Uingereza zenye thamani ya Dola
milioni 150, kiwango ambacho ni kidogo sana na tunahitaji kufanya
biashara zaidi" Alisisitiza Dkt. Mpango.
Alielezea
hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua kuimarisha uchumi wa
viwanda na kuelezea changamoto kubwa ikiwa na namna ya kuendeleza kilimo
kwa ajili ya kupata malighafi za viwanda na kuwainua wananchi kiuchumi
kwa kuwa kilimo ndicho kinaajiri idadi kubwa ya Watanzania.
Dkt.
Mpango alitoa wito kwa Serikali ya Uingereza kuwekeza zaidi katika
viwanda vitakavyoongeza thamani ya bidhaa mbalimbali ikiwemo kujenga
viwanda vya kutengeneza matrekta na zana nyingine za kilimo, kusindika
bidhaa za mazao ya wakulima pamoja na kuwekeza katika sekta za kuongeza
thamani ya madini na nishati ya umeme.
Dokta
Mpango aliwaeleza Wabunge hao kwamba hivi sasa Serikali imepiga hatua
kubwa kiuchumi na kuishukuru Uingereza kwa mchango mkubwa inaoutoa
kusaidia Elimu, Lishe, Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma na afya
kwa upande wa lishe, uwekezaji ambao kwa pamoja umefikia zaidi ya paundi
milioni 180.
Kwa
upande wake, kiongozi wa Wabunge watano waliomtembelea Waziri wa Fedha
na Mipango, Mheshimiwa David Linden, amesema wamefurahishwa na namna
Tanzania inavyopiga hatua kubwa kimaendeleo na kudhibiti vitendo vya
rushwa.
Amesema
kuwa wameridhishwa na kiwango cha miradi wanayoifadhili katika sekta ya
elimu na afya hususan masuala ya lishe kwa watoto na kwamba nchi yao
itaendelea kuisaidia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake kiuchumi na
kijamii
Wabunge hao wapo nchini tangu Jumapili iliyopita na wanatembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza.