Bukobawadau

VIONGOZI WANNE WA CUF LIPUMBA WAFA KWA AJALI

Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahamika kwa jina moja Uredi.
Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
Next Post Previous Post
Bukobawadau