Bukobawadau

AJALI MBAYA YATOKEA LEO MULEBA

Watu watano wamefariki dunia hii leo majira ya saa 12 asubuhi kwa kuungulia ndani ya gari aina ya Hiece iliyopata ajali baada ya kugongana na semi aina ya scania mpakani mwa kijiji cha Kyamyorwa na Kasharunga wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richard Ruyango amethibitisha kutokea ajali hiyo na kwamba baada ya magari hayo kugongana dreva, tingo na abiria watatu walishindwa kutoka kutokana na milango ya hiece kubanana.

Amesema kwa taarifa alizopata kutoka eneo la tukio ni kwamba dreva aliyekuwa akiendesha hiece hiyo yenye namba za usajili T. 470 DEY ametambulika kwa jina la Magesa Maselele mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa kijiji cha Nyakabango wilayani Muleba na maiti nyingine hazijatambulika
Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Kyamyorwa kata ya kasharunga Jonathani Mathayo amesema ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu ya kutoka muleba kwenda biharamulo eneo la daraja la katelela kwenye kitongoji cha kishenye kijijini humo na hiece iligongana na semi aina ya scania yenye namba za usajili T701 BBP iliyokuwa ikitokea DSM kuelekea bukoba mjini.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi naye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo ni mwendo kasi wa hiece na ilikuwa katika harakati za kukwepana na loli la mizigo na ajali kutokea na magari yote yameteketea kwa moto.
#bukobawada
Next Post Previous Post
Bukobawadau