MSHINDI WA TISA WA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA APATIKANA TUNDURU
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh Juma Homera (Kushoto) akiwa na MWakilishi
wa Tatu Mzuka Bi Kemi Mutahaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiuma
Bw. Joseph Mtuma Wakimpongeza Mshindi wa 9 wa Tatu Mzuka Jackpot Bw
Fulko Hyera, kijijini Kiuma, Tunduru
Mshindi wa 9 wa Tatu mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, Mwalimu wa
shule ya sekondari Kiuma,akifurahia alipo kabithiwa cheki ya Milioni 60
kutoka Tatu Mzuka kijijini kwake Kiuma, Wilaya ya Tunduru.
Bw. Fulko Hyera and Mke wake Sigsberta Haule mbele ya duka lao
kijijini Kiuma wakisherekea kipato cha Million 60 kutoka Tatu Mzuka.
Mshindi wa droo ya tisa ya Tatu Mzuka amepatikana Jumapili hii ya Oktoba 1, 2017. Mshindi huyu amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 na ni Bwana Fulko Hyera, mkazi wa kiuma, wilayani Tunduru
Ushindi huu wa Bw.Hyera unaonesha namna Tatu Mzuka inavyobadili maisha ya wananchi wa Tanzania sio tu wa mjini bali na vijijini pia. Bw. Hyera ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Kiuma.
Bw Hyera alisema “Katika muda wangu wote, sikuwaza kuwa na hela hizi. Kama familia zetu nina majukumu mengi yakutimiza na sasa nitakuwa na uwezo wa kusaidia familia. Sasa nimeamua kuanza biashara, niajiri wengine na kuongeza fursa za vijana”
Kumkabidhi cheki Bw Hyera, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Juma Homera alimkabidhi cheki mshindi kwenye tulio lilio andaliwa na Tatu Zuka kijijini Kiuma, Tunduru.
Mheshimiwa Homera alikuwa ana machache ya kusema licha la kumpongeza Bw. Hyera alimuhusia “ Hizi ni hela nyingi sana. Lazima uwe na malengo kamili and pia hii itakupa fursa nyingine ya kusaidia jamii.” Amewapongeza sana Tatu Mzuka kwa kuchangia kubadili maisha ya watu tena ya mwana Tunduru.
Licha ya ushindi huo, Bw. Hyera alipata pia fursa ya kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao pia walijishindia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa kila mmoja. Mmoja ya rafiki zake Bi.Marianna Haule ambaye mara nyinji anamuuguza mama yake, ndio alichaguliwa. “Nilimuwaza Marianna ili nijaribu kumpa haueni akiwa anamuuguza mama yake.” Alieleza Bw. Hyera
Tatu Mzuka hadi leo imetoa zaidi ya Billion 2 kwa washindi na wamepata zaidi ya washindi 900,000.
Wiki hii Jumapili kutakuwa na Million 80M.Namna ya kucheza promosheni ya Tatu Mzuka Unatakiwa kwenda kwenye sehemu ya fedha kwenye simu yako na kuchagua Lipana kwa M-Pesa au mitandao mingine. Kisha unaingiza namba zako 3 za bahati katika sehemu inayoonekana. Kisha weka kiwango chako cha fedha kuanzia shilingi 500/- hadi 30,000/-
Kwa kuanzia kiasi cha shilingi 500,TatuMzuka inatoa fursa ya kushinda hadi shilingi milioni 6 ndani ya saa 24 kwa siku. Chagua namba tatu za bahati kuanzia 0-9 kisha zitume zikiambatana na pesa ya ushiriki kuanzia shilingi 500/. Ukishinda namba zako zote tatu utajinyakulia fedha mara 200 ya ile uliyocheza huku pia kila shilingi 500 unayocheza inakupa nafasi ya kushiriki droo inayochezwa kila wiki ambayo inakupa fursa ya kushinda hadi shilingi milioni 70.
Ili kupata taarifa zaidi kuhusu washindi wa Tatu Mzuka angalia Televisheni za Clouds na TV1 kila Jumapili kuanzia saa Tatu na Nusu Usiku.