UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja
wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Yapi
Merkezi Abdullah Kilic,
anayejenge reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani
Pwani
Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mhandisi Maizo Mgedzi,
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka
Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani,
inayojengwa usiku na mchana.
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah
Kilic, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR),
kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa, katika eneo la Soga, mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akimpongeza mwanamke
anayeendesha mtambo wa kutengeneza tuta la reli ya kisasa (SGR), Bi Miriam Juma
alipomkuta saa 4 za usiku akichapa kazi katika eneo la Soga, mkoani Pwani.
Muonekano wa Mitambo
ya kisasa inayojenga Reli ya Kisasa (SGR),
kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga mkoani Pwani,
inayojengwa kwa saa 24.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezungumzia umuhimu
kwa wafanyakazi wote waliopata fursa ya kujenga reli ya kisasa (SGR) kufanya
kazi kwa moyo na uzalendo mkubwa ili kuandika historia katika maendeleo ya
Tanzania.
Profesa Mbarawa
amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na
mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro
yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa
kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii
hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof.
Mbarawa.
Amewataka viongozi
wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati
wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo
kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha
amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha
wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo
katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu
kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni
wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na
wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Naye Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo
imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi
huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.
Takribani
shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu
ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha
treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa
usafiri wa reli hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano