WASANIFU MIRADI YA UJENZI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa,
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Eng. Jackson Masaka pamoja na viongozi
wengine wa wilaya hiyo, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi China Henan International Corporation anayejenga daraja
la Sibiti lenye urefu wa mita 82 na barabara za maingilio kwa kiwango cha
changarawe zenye urefu wa KM 25, alipokagua ujenzi wa miradi hiyo mkoani
Singida.
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo, akifafanua jambo kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias
Kwandikwa (wa pili kulia), alipokagua ujenzi wa daraja la Sibiti lenye urefu wa
mita 82 na barabara za maingilio kwa kiwango cha changarawe zenye urefu wa KM
25, mkoani Singida
Mhandisi Mshauri Mr.
Sunil Singh, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, uwekaji zege katika moja ya boksi kalvati
kubwa linalojengwa katika barabara za maingilio ya daraja la Sibiti, mkoani
Singida.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (katikati), akioneshwa na Mhandisi Mshauri Mr. Sunil Singh (kulia), nguzo zilizojengwa kushikilia daraja la sibiti, alipokagua ujenzi wake jana, mkoani Singida. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa,
akizungumza na wananchi wa kata ya Mpambala wilayani Mkalama, wakati alipokagua
ujenzi wa daraja la Sibiti lenye urefu wa mita 82 na barabara za maingilio kwa
kiwango cha changarawe zenye urefu wa KM 25, mkoani Singida.
Muonekano wa nguzo tatu zitakazoshikilia Daraja la Mto Sibiti lenye
urefu wa Mita 82 na upana wa mita 10.5. Daraja hilo ni kiungo muhimu kwani litaunganisha
Wilaya ya Iramba na Mkalama mkoani Singida na Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano