SERIKALI YASAINI MIKATABA MINNE YA UJENZI WA BARABARA.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, pamoja na viongozi
wengine wa Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Bi.
MarieHellen Minja, wakishuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya
mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402)
lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini,
Mhandisi Patrick Mfugale, akibadilishana nyaraka za mkataba mara baada ya
kusaini na Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo Bw. Chen Xianghua leo
jijini Dar es salaam, atakayejenga
barabara ya Usesula hadi Komanga km 108.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama ishara ya shukrani kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni kwake, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama ishara ya shukrani kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni kwake, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia
ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimkabidhi zawadi
Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. MarieHellen Minja, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji
saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda
na Mbinga – Mbaba Bay zenye jumla ya (kilomita
402), jijini Dar es Salaam.
SERIKALI
YASAINI MIKATABA MINNE YA UJENZI WA BARABARA.
Serikali imesaini mikataba minne na kampuni nne
za ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 702 kwa ujenzi wa
kilomita 402.
Tukio hilo la kusaini mikataba hiyo
limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Mandeleo ya Afrika
(AfDB), MarieHellen Minja, wabunge ambao miradi hiyo ya Barabara itapita
majimboni mwao, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakandarasi walioshinda
zabuni.
Akizungumzia utiaji saini huo, Waziri Mbarawa amesema fedha hizo
zitatumika katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tabora (Usesula)- Koga hadi Mpanda
yenye urefu wa kilomita 335 na kilomita 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay mkoani
Ruvuma.
Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa
barabara hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na ahadi za
Rais John Pombe Magufuli wakati wa
kampeni.
Aidha, Waziri Mbarawa ametumia nafasi
hiyo kuwataka wakandarasi walioshinda zabuni kujenga barabara zenye ubora na
viwango kwa kuzingatia muda wa ujenzi.
Profesa Mbarawa ameongeza kuwa nia ya
Serikali ni kuona ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020.
"Naomba TANROADS msimamie ujenzi
wa barabara yenye ubora kwani wakandarasi wengi ni wajanja na ikitokea mtu
ameharibu asipewe nafasi kabisa ya ujenzi wa barabara hapa nchini,"
amesema Waziri Mbarawa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa wakandarasi waliopewa kazi
wametokana na uchambuzi mkubwa uliofanyika kati ya wakandarasi 129
waliojitokeza mwaka 2016 kuomba zabuni za ujenzi wa barabara hizo.
Mhandisi Mfugale amefafanua kuwa ili
kurahisisha ujenzi wa barabara hizo wamegawa kwa wakandarasi wanne ambapo
barabara ya Usesula hadi Komanga kilomita 108 itajengwa na Kampuni ya Jiangxi
Geo-Engineering Group Corporation Limited ya China kwa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni
158 na itajengwa kwa miezi 36.
"Komanga hadi Kasinde kilomita
108 itajengwa na Mkandarasi Kampuni ya China Wu Yi Co. Limited kwa zaidi ya
sh.billioni 140 na Kasinde hadi Mpanda kilomita 105 Mkandarasi Kampuni ya China
Railway Seventh Group Co.Ltd kwa sh. Bilioni 133," amesema Mhandisi
Mfugale.
Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay
kilomita 67 inajengwana Mkandarasi China Henan
International Corporation Group Co.Ltd (Chico) kwa sh. Bilioni 129.
Amesema TANROADS imejipanga kusimamia
ujenzi huo kwa kufuata viwango vinavyohitajika vya ujenzi wa barabara nchini.
Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. Minja
amesema ofisi yake itaendelea kutoa mchango kwa serikali katika ujenzi wa
miundombinu mbalimbali nchini pale watakapo hitajika.
Bi. Minja amesema kuwa matarajio ya AfDB ni kuona Tanzania inapata
maendeleo kwa haraka na njia rahisi ni kupitia miundombinu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye barabara ya Tabora hadi Mpanda inapita jimboni
kwake ambapo amesema kuwa ujenzi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi na
kijamii.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, amesema barabara hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya
Tanzania, Msumbiji na Malawi.
Amesema kuwa Nyasa ina vivutio vingi
vya utalii hivyo ujio wa barabara hizo utakuwa njia rahisi ya kuwafikisha
watalii eneo hilo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.