Bukobawadau

HAFLA YA MWAKA YA 'LUGOYE DAY' YAFANA !

 Katika picha ya pamoja ni Wanachama wa Lugoye Social Club na Logoye 'Lugoye Women Group' walioshiriki hafla ya mwaka 2018 ya 'Lugoye Day' Iliyofanyika Kijijini Kwelima- Inshunju kwa Mzee Josephat Byemerwa.
 Wanachama wa Umoja ujulikanao kama Lugoye Social Club wanaozaliwa katika vijiji vya Ishozi ,Gera na Inshunju na makazi yao yakiwa Jijini Dar es Salaam wameendelea kusherekea sherehe zao za kila mwaka ambalo limekuwa tukio la kuambatana na matendo ya huruma kwa kusaidia jamii inayo wazunguka hususani katika Vijiji Vyao.
Ambapo kwa mwaka huu wameweza kukabidhi Photocopy Mashine katika Shule ya msingi Kyelima na kwa upande wa wanawake wanachama wa Lugoye 'Lugoye Women Group' wametoa msaada wa kompyuta na Printer.
Mapema mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya shule ya msingi Kyelima iliyopo kata Inshunju.
 Matukio ya awali wakati wa makabidhiano ya zawadi hizo Wanachama wa Lugoye Social Club na Wajumbe wa kamati ya shule ya Msingi Kyelima.
Mwenyekiti wa Lugoye Group akiongea na Mwanahabari Benson wa Clouds Media


Baadhi ya Wanachama wa Lugoye Social Club walioweza kuhudhuria hafla hiyo
Pata muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri nyumbani kwa Mzee Josephat Byemerwa hafla ya mwaka ya Lugoye Day.




 Mzee Matambula pichani katika Utambulisho
 Mlangira Focas Lutinwa wakati wa Utambulisho
 Mzee Josephat Byemerwa mwenyeji wa hafla hiyo akitoa utambulisho kwa familia yake
 Mzee Josephat Byemerwa akiendelea kutoa utambulisho kwa watoto wake waliowedha kushiriki hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake Kijijini Inshunju tarehe 27/12/2018.
Mzee Justus Rweyemamu na Prof.Kahamba wanachama wa Lugoye Social Club wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Diwani Msafiri wa Kata Inshunju akikabidhiwa Computer na Printer kutoka kwa wanachama wa Lugoye Women.
Katika picha ya pamoja Vijana wa familia za WanaLugoye.
Kwa namna ya pekee Mzee Josephat Byemerwa akitoa neno na utambulisho kwa Baba yake Mlezi.
Mzee anakabidhiwa kipaza sauti kwa ajili ya kutoa neno
Muendelezo wa matukio ya picha #haflayalugoyeDay
Mchungaji akitoa utambulisho kwa mke wake


Ni muda wa kupata huduma safi ya msosi ulioandaliwa wakati wa hafla hiyo.








Burudani ikiendelea kuchukua kasi 
Ni mwendo wa burundani ya ngoma ya Asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya wanawake walioshiriki hafla hiyo
Ni mwendo wa burudani ya ngoma ya asili ya #buhaya


Muendelezo wa  matukio ya picha.
 Burudani ya aina yake na ya kulidhisha kutoka kwa kikundi cha Wawindaji wa asili wa Inshunju
Mwenyekiti wa kikundi cha Asili cha Wawindaji akitoa neno
 Mlangira Focas Lutinwa akionyesha kuguswa na mambo ya Asili kutoka kwa wawindaji hao
 Muonekano wa dhana za kikundi cha wawindaji wa asili 'Abaigi'


 Burudani ikiendelea ukumbini

 Mh.William Lutta Diwani wa kata ya Ishozi
Sala ya kufunga shughuli hii.
Tunatoa shukrani za dhati kwa waandaaji wa hafla hii ya LUGOYE DAY 2018 Mr & Mrs Josephat Byemerwa baraka za Bwana ziwe nanyi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau