BALOZI DR KAMALA KATIKA MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO YA JIMBO LA NKANGE 2019
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwahutubia wadau waliohudhuria Mkutano wa wadau wa maendeleo ya Jimbo la Nkenge uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashaui ya Missenyi tarehe 3/01/2019.
Hotuba katika Mkutano wa Wadau
Waheshimiwa Wadau!
Ninayo
furaha kubwa kuwakaribisha leo hii kushiriki Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya
Jimbo la Nkenge. Karibuni sana na ahsante sana kuhudhuria.
Namshukuru
Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana hapa leo hii.
Waheshimiwa Wadau!
Naomba
niwatakie heri ya mwaka mpya. Kama
mnavyofahamu mwaka huu umeitwa
Birug’omumpiita. Jina la mwaka huu linaenda sambamba na falsafa ya Hapa
Kazi Tu! Kikao chetu cha leo kitatusaidia sana kuweka mipango na kubainisha
vipaumbele vya kuzingatia kusukuma gurudumu la maendeleleo
Waheshimiwa Wadau!
Kama
mnavyofahamu mwaka jana katika Wilaya yetu walizaliwa Watoto mapacha Anisia na Marines waliokuwa wameungana. Baada
ya taarifa hizo kuandikwa katika vyombo vya habari, Serikali ya Saudi Arabia
iliamua kuchukua jitihada za makusudi za kufanya upasuaji wa kutenganisha
Watoto hao. Tarehe 23/12/2018 upasuaji huo ulifanyka huko Saudi Arabia kwa
mafaniko makubwa. Upasuaji huo hulijumuisha Madaktari Bingwa 32 na wauguzi 120. Upasuaji huo ulioneshwa katika vyombo
vya habari na ulichukua masaa 13. Nachukua fursa hii kumshukuru mfalme wa Saudi
Arabia kwa kugharamia upasuaji huo uliogharimu wastani wa fesha za Kitanzania
bilioni moja na milioni mia tano. Aidha, namshukuru pia Balozi wa Tanzania
Saudi Arabia, Balozi Hemed kwa kuratibu na kuhakikisha upasuaji huo
unafanikiwa.
Nawashukuru
pia Madaktari na Wauguzi wote wa hapa Tanzania kwa huduma zao zilizowesha
kuwandaa Watoto waliokuwa wameungana na hatimae kuwezesha upsuaji huo kufanyika.
Vilevile nawakukuru Watanzania na Wanankenge kwa sala zenu zilizowezesha
kufanikiwa kwa upasuaji wa mapacha hao.
Waheshimiwa Wadau!
Lengo
kuu la mkutano huu ni kujadili maendeleo ya Nkenge na kuweka mikakati ya
kusukuma gurudumu la maendeleo. Katika
kikao cha Wadau kilichotangulia kabla ya hiki
tulijadili na kupitisha Mkakati
wa Kuimarisha Soko la Haki la Kahawa (Far Trade) kwa Maendeleo ya Wakulima wa Kahawa Wilayani
Missenyi. Baada ya kikao chetu, Serikali ilitoa msukumo mkubwa katika
kuimarisha na kuendeleza zao la kahawa. Pia kwa mara ya kwanza, Serikali
imeelekeza mnada wa kahawa uwe unafanyika hapa Kagera. Ni matarajio yangu
maelekezo ya Serikali yatasaidia sana kuimairsha zao la kahawa.
Waheshimiwa Wadau!
Katika
kikao chetu cha leo tutatathimini mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM
katika miaka mitatu kuanzia mwaka 2016, 2017 hdi 2018. Pia tutabainisha maeneo ya kuongeza msukumo
katika kuharakisha maendeleo ya Jimbo letu la Nkenge.
Waheshimiwa
Wadau!
Kama mnavyofahamu
mgogogro wa mipaka kati ya Ranchi ya Missenyi na vijiji vinavyopakana na Ranchi
hiyo umechukua muda mrefu. Manamo tarehe 10/05/2018 nilimuandikia Mhe. Waziri
Mkuu na kumuomba asaidie kumaliza mogogoro huo. Mhe. Waziri Mkuu amaechukua
hatua muhimu za kusaidia kumaliza mgogoro huo. Maelekezo yametolewa kwa Wizara
zote zinazohusika na mgogoro huo na ni matarajio yangu tutapata ufumbuzi wa
kudumu wa mgogoro huo.
Waheshimiwa
Wadau!
Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Bajeti 2017/18 lilishauri kuwa kuwa
migogoro yote ya mipaka ya hifadhi na wananchi itaamuliwa kwa ushirikishwaji wa
wadau wote muhimu wakiwepo viongozi wa Serikali, wanasiasa, wananchi na taasisi
zinazohusika na uhifadhi. Aidha, Mkurugenzi wa Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na
maendeleo ya Makazi ndiye mwenye dhamana ya kisheria ya kuonesha mipaka yote ya
Ardhi nchini iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria. Ni matarajio yangu kuwa
ushauri wa Bunge kwa Serikali utatusaidia sana kupata ufumbuzi wa kumaliza
igogoro ya mipaka kati ya Msitu wa Minziro na vijiji vinavyozunguka msitu huo
na pia tutapata ufumbuzi wa na wa
migogoro ya mpaka kati ya Hifadhi za Taifa za Rusiina, Kiikuru na vijiji
vinavyozunguka hifadhi hizo.
Waheshimiwa
Wadau!
Mojawapo ya kazi
muhimu za Bunge ni kutunga sheria. Hivi karibuni kuna miswada mitano ya sheria
ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Muswada ukisomwa kwa mara ya kwanza
bungeni unatoa fursa kwa wadau kuanza kutoa maoni yao. Natoa wito kwa wadau wa
maendeleo ya Nkenge kusoma miswada hiyo na kunipatia maoni yenu ili wakati wa
kutunga sheria ukifika niweze kuwasilisha maoni yenu.
·
Miswada
hiyo ya sheria ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza ni Pamoja na: Muswada wa
Sheria na 4 wa madailiko ya Sheria Mbalimbalimbali, 2018
Muswada huu unalenga kufanya mabadilko
katika Sheria ya Serikali za mitaa,\
·
The
Tanzania Meteorological Authority Bill, 2018
Muswada huu unalenga kuanzisha wakala wa
kuratibu hali ya hewa. Pamoja na mambo mengine muswada huu unabainisha adhabu
zitakazotolewa kwa makosa mbalimbali kwa wale watakaovunsja sheria husika.
Sheria hii itanya kazi Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
·
The
Land Transport Regulatory Authority Bill, 2018
Muswada huu utaanzisha Wakala wa Usafiri katika
nchi kavu
·
The
Politica Parties (Amendments Bill, 2018 na
·
The
Water Supply and Sanitation Bill, 2018
Taarifa ya
Mafanikio
Miswada
niliyobainisha hapo juu inapatikana mabadiliko zinapatikana katika tovuti ya
Bunge inayopatikana katika anwani parliament.go.tz
Waheshimiwa
Wadau!
Kuanzia mwaka 2016
hadi 2018 kuna mafanikio mengi yaliyotokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Katika Mkutano huu wa Wadau naomba nitaje baadhi ya mafanikio ya yaliyotokana
na utelekezaj wa Ilani ya CCM katika ngazi ya Halmashauri ya Missenyi
Jedwali na II:
Baadhi ya Mafanikio ya Utekelezaji wa ilani ya CCM katika Ngazi ya Halmashauri
ya Wiilaya ya Missenyi
Na.
|
Mafanikio
|
Matarajio
|
1.
|
Asilimia ya
upatikanaji dawa imeongezeka kutoka asilimia 68 mwaka 2015/16 hadi kufikia
asilimia 92 mwaka 2017/18
|
Bado kuna baadhi
ya dawa ambazo haziko kwenye kundi za dawa mahimu. Zinakosekana kwenye vituo
vya kutolea huduma.
|
2.
|
Vituo vya
kutolea huduma za afya 22 vimeboreshwa kwa kupaka rangi, kujebga vichomea
tala na placenta pit
|
Bado vijiji 45
havina zahanati na kata 17 hazina vituo vya afya
|
3.
|
Ongezeko la
wanachama mfuko wa afya ya Jamii CHF kutoka asilimia 8 mwaka 2015/16 hadi
kufikia asilimia 30 2017/18
|
Kasi ndogo ya
wananchi kujiunga na CHF. Kutekelezwa kwa chf iliyoboresha kutasaidia
kuboresha huduma za afya
|
4.
|
Jumla ya wazee 6,082
kati ya wazee 11,514 waliotambuliwa wamepewa vitambulisho sawa na asilimia
52.8
|
Wazee wote
waliotambuliwa watapatiwa kadi za matibabu bure
|
5.
|
Ujenzi wa kituo
cha Afya cha Kabyaile
|
Kuboresha huduma
za kituo cha afya cha Kabyaile
|
6.
|
Kiwango cha
wagonjwa wa malaria kimepungua kutoka asilimia 17 mwaka 2015/16 hadi kufikia
asilimia 12 mwaka 2017/18
|
Kuendelea kutoa
elimu juu ya matumizi bora ya vyandarua
|
7.
|
Kiwango cha
maambukizi ya virusi vya ukimwi kimepungua kutoka asilimia 3.5 mwaka 2015
hadi asilimia 2 mwaka 2018
|
Kupunguza
maambikizi mapya ya ukimwi na kuendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya
ukimwi na kuwaanzishia dawa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
|
8.
|
Kiwango cha
utoaji chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 85 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 92 mwaka 2018
|
Kuhakikisha wote
wanaostahili kupewa hanjo wanapata chanjo
|
9.
|
Kupata milinioni
400 kutoka Serikali kuu za kuboresha kituo cha afya Bunazi
|
Kituo cha Afya
Bunazi kuendelea kuboreshwa
|
10.
|
Halmashauri kwa
kushirikiana na Kituo cha Utafiti
Maruku imefanikiwa kusambaza miche bora ya kahawa 32,200 kwa wakulima
|
Mahitaji ya
miche bora ya kahawa bado ni makubwa. Halmashauri itaanzisha vitalu
|
11.
|
Kwa kutumia mfuko wa Mbunge Halmashari iliweza kusambaza
mbegu bora za Alizeti kilo 240 sawa na ekari 34 ili kuhamasisha kilimo cha
Alizeti
|
|
12.
|
Kuanzishwa kwa
mazao mapya ya kilimo kwa nia ya kuongeza kipato cha mkulima. Mazao ya
Alizeti, Chia Seeds na Soya yameanza kulimwa katika Wilaya ya Missenyi.
|
|
13.
|
Halmashauri
imeweza kufanya sensa ya wakulima wa kahawa na kupata jumla ya wakulima
14,264 waliolima jumla ya ekari 4,557 yenye miti ya kahawa aina ya arabika
22,018 na miche ya robusta 1,483,513
|
|
14.
|
Kukamilika kwa
mradi wa maji Kilimilile ambao umegharimu 400,000,000/=
|
|
15.
|
Mradi wa maji
Rukurungo umekemilika na umegharimu 424,547,000/=
|
|
16.
|
Mradi wa maji
Nyabihanga wa zisima vifupi viwli umekamilika na unafanya kazi kwa gharama ya
214,392,000/=
|
|
17.
|
Mradi wa maji wa
Igurugati umegharimu 290,297,244/=
|
|
18.
|
Mradi wa Maji wa
Kenyana kisima kirefu umegharimu 328,507,000/=
|
|
19.
|
Mutukula mradi
wa maji mradi umegharimu milioni 653,288,886
|
|
20.
|
Bubale, Kibeo na
Bwoki. Uchimbaji wa visima unaendelea.
Mradi umegharimu 142,602,665
|
|
21.
|
Kakunyu mradi
utakaogharimu 779,296,100/= unaendelea kujengwa
|
|
22.
|
Bugango, mradi
unaendelea kujengwa na utagharimu milioni 782,234,200/=
|
|
23.
|
Ruzinga, Ruhija
na Mgongo mradi utagharimu 314,047,681 unaendelea kujengwa
|
|
24.
|
Mradi wa maji Kibeo
ambao utagharimu 123,404,000/= unaendelea kujengwa
|
25.
|
Mradi wa maji ya
mto Kagera kwa ajili ya Kyaka na Bunazi. Maandalizi ya kuanza kutekeleza
mradi yanaendelea. Mhandishi Mshauri mpya amaepatikana. Kibali cha kuanza kazi kinasubiriwa kutoka
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
|
|
26.
|
Kuongezeka
vyumba vya madarasa kutoka 521 mwaka 216 hadi 650 mwaka 2018
|
|
27.
|
Kuongezeka
nyumba za walimu kutoka 192 mwaka 2016 hadi 205, mwaka 2018
|
|
28.
|
Kuonezeka
matundu ya vyoo kutoka 887 2016 hadi 915 2018
|
|
29.
|
Madawati
kuongezeka kutoka 15,269 mwaka 2016 hadi 19,786 mwaka 2018
|
|
30.
|
Kiwango cha
kufaulu darasa la saba kimeongezeka kutoka asilimia 78.8 mwaka 2016 hadi 83.7
mwaka 2018
|
|
31.
|
Kiwango cha
kufaulu darasa la nne kimeomgezeka kutoka asilimia 86 mwaka 2015 hadi
asilimia 88 mwaka 2017
|
|
32.
|
Ufaulu wa
mitihani kidato cha pili umeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi
asilimia 84.5 mwaka 2017
|
|
33.
|
Ufaulu wa
mitihani kidato cha nne umeongezeka kutoka asilimia 62 mwaka 2015 hadi
asilimia 100 mwaka 2018
|
|
34.
|
Vyumba 31 kati
ya 66 vya maabara vimejengwa na vinatumika
|
Jedwali namba II limebainisha
baadhi tu ya mafanikio. Mafanikio mengine nimewaachia wadau wa maendeleo waweze
kuyabainisha. Aidha, Meneja wa TANESCO wa
wilaya ya Missenyi atabainisha mafanikio katika sekta ya nishati, meneja wa
TARURA Missenyi naye atabainisha mafanikio katika Sekta ya barabara na Meneja
wa MSD atabainisha mafanikio katika upatiakanaji na usambazaji wa madawa katika
Wilaya ya Missenyi. Aidha, Bomba la Mafuta kutoka Uganda kuelekea Tanga nalo
litachangia sana katika kuongeza mapato ya Taifa na kukuza uchumi
Waheshimiwa
Wadau!
Mojawapo ya ahadi
niliyotoa ni kutafuta fedha za kutoa mafunzo maalum ya kuwawezesha vijana na
akina mama kuweza kujiajiri. Naomba niwajulishe kwamba hatimae tumepata mdau
ambaye atatoa mafunzo kwa vijana na akina mama wasio chini ya mia tano ili
waweze kujiajiri na kuongeza fursa za kipato. Mafunzo haya yataanza kabla ya
mwaka wa fedha wa 2018/19 kumalizika. Taarifa zaidi nitawajurisha mafunzo
yakikaribia kuanza.
Waheshimiwa
Wadau!
Ahsante sana
kushiriki katika Mkutano huu wa Wadau wa Maendeleo ya Jimbo la Nkenge. Na sasa
nawakaribisha kutoa maoni yenu yenye lengo la kubainisha mikakati mbalimbali ya
kusaidia kuonegeza kasi ya maendeleo katika jimbo la Nkenge. Kwa Pamoja
tunaweze! Ahsante sana kunisikiliza.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akikabidhi pump ya kusukuma maji Bi Theopista John wa Kijiji cha Bugogora ,Balozi Kamala ametekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa kikundi cha 'Nkenge Youth Group',kikundi kinacho jihusisha na kilimo cha mbogamboga maeneo ya Bugorora kando kando ya mto Kagera.
Mdau wa maendeleo akimsikiliza kwa makini mbunge wake.
Baadhi ya wadau wakiendelea kushiriki mkutano huo
Ndugu Jovin Barongo Kaimu Meneja wa TARURA halmashauri ya Wilaya Missenyi
Eng. Idd Makung'uto Kaimu Mhandisi Maji halmashaui ya Wilaya Missenyi
Mh.Tegamaisho Mwenyekiti wa Halmashauri Missenyi.
Katibu wa CCM Wilaya Missenyi Mama Mbohe katika picha na Mkurugenzi wa Halmashauri Missenyi
Balozi Dr.Kamala akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya Missenye ,Mama Mboha.
Mdau akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge
Muendelezo wa matukio ya picha Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Wa Jimbo la Nkenge.
Taswira mbalimbali wakati mkutano ukiendelea
Ndugu Dominic Lumato Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya Missenyi akiongea kuhusu mchakato wa usambazaji wa Umeme Vijijini REA unavyoendelea Wilayani Missenyi
Dr. Joachim Mchunguzi Mazima akiendelea kushiriki mkutano huo ulio andaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala
Mzee Leopold Rwizabdekwe pichani Mkazi wa Kijiji Katendaguro Kata Bugandika
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa MSD kutoka MSD -Muleba ,Bw. Masatu Kalendero
Dr. Habasi Mganga Mkuu wa Wilaya Missenyi
Mh.William Osward Rutta Diwani wa Kata Ishozi
Ndugu George Rubaiyuka Joseph Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari halmashauri Missenyi akitolea hoja ufafanuzi kuhusu elimu.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Nkenge, Lengo ikiwa ni kutathimia shughuli za maendeleo na kubainisha masuala ya kupewa kipaumbele mwaka 2019.
Baadhi ya wadau wakiendelea kushiriki mkutano huo
Ndugu Jovin Barongo Kaimu Meneja wa TARURA halmashauri ya Wilaya Missenyi
Eng. Idd Makung'uto Kaimu Mhandisi Maji halmashaui ya Wilaya Missenyi
Mh.Tegamaisho Mwenyekiti wa Halmashauri Missenyi.
Katibu wa CCM Wilaya Missenyi Mama Mbohe katika picha na Mkurugenzi wa Halmashauri Missenyi
Balozi Dr.Kamala akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya Missenye ,Mama Mboha.
Mdau akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge
Muendelezo wa matukio ya picha Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Wa Jimbo la Nkenge.
Taswira mbalimbali wakati mkutano ukiendelea
Ndugu Dominic Lumato Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya Missenyi akiongea kuhusu mchakato wa usambazaji wa Umeme Vijijini REA unavyoendelea Wilayani Missenyi
Dr. Joachim Mchunguzi Mazima akiendelea kushiriki mkutano huo ulio andaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala
Mzee Leopold Rwizabdekwe pichani Mkazi wa Kijiji Katendaguro Kata Bugandika
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa MSD kutoka MSD -Muleba ,Bw. Masatu Kalendero
Dr. Habasi Mganga Mkuu wa Wilaya Missenyi
Mh.William Osward Rutta Diwani wa Kata Ishozi
Ndugu George Rubaiyuka Joseph Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari halmashauri Missenyi akitolea hoja ufafanuzi kuhusu elimu.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Nkenge, Lengo ikiwa ni kutathimia shughuli za maendeleo na kubainisha masuala ya kupewa kipaumbele mwaka 2019.