MUSHEMBA TRINITY SCHOOL – Nyota inayong’ara Tanzania.
Mushemba Trinity school ni shule ya kutwa
na bweni inayomilikiwa na Mushemba Foundation iliyoanzishwa takribani miaka 8 na mwanzilishi wake Bw.
Josephat Mushemba ambaye pia ndiye mkurugenzi mkuu wa
shule hii.
Bw. Josephat Mushemba pichani Mkurugenzi wa Shule ya Mushemba Trinity iliyopo Manispaa ya Bukoba akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo waliofaulu vizuri kwa mwaka 2018 wengi wao wakiwa na daraja ”A” na kuipa shule hiyo nafasi ya pili kiwilaya.
Mwaka
juzi baada ya matokeo ya mtihani wa kitaifa
ya darasa la nne kutoka ,
nilipata nafasi ya kutembelea shule na
kuandika makala inayosema ”
Mushemba Trinity” tunda
linalochipuka na hapo ilikuwa imechukua
nafasi ya 3/13 kiwilaya na 5/350
kimkoa na 13/5875 kitaifa, hapo ilikuwa mwaka 2016.
Baadae mwaka 2017 , nilikuwa katika kazi zangu ,
nikasikia kuwa shule
imefanya vizuri kwa mara ya pili na kuwa
ya 1/11 kiwilaya , 5/255 kimkoa na 13/5123, Na kwa ushindi huu shule ilikuwa ikishindana na
shule nyingine ambazo ziko katika kundi
la watoto wasiozidi 40 darasani, ambapo kiukweli shule za idadi hii sio nyingi mno.
Mwaka 2018 shule hii ilikuwa kwenye kundi
la shule ambazo zina watoto zaidi ya 40
darasani ambapo shule zenye idadi hii ni
nyingi, hapo tena hamu yangu ilikuwa
kubwa zaidi kujua matokeo yatakuwaje.
Punde
matokeo yalipotoka ya mwaka
2018,nilikimbilia kwenye mtandao kuangalia matokeo ambapo
kwa mara ya tatu shule ya Mushemba Trinity
iliendelea kung’ara zaidi. Shule imekuwa ya
2/33 kiwilaya, ya 15/791 kimkoa na 69/13182
kitaifa ambapo shule iliingia katika kundi la shule bora kitaifa, kwa maana ya Tanzania nzima.
Tarehe 10/01/2019 , Mkurugenzi wa shule Bw. Josephat Mushemba , alifanya sherehe ya
kuwapongeza wanafunzi ambao wengi wao walishinda kwa daraja ”A” nami nilipata nafasi ya
kuhudhuria sherehe hiyo.
Shule
imejificha kidogo prmbeni mwa barabara kuu kuelekea Maruku na imezungukwa na
mazingira yaliyopambwa na kupandwa maua.
Moja kati ya Jengo la Bweni la shule hiyo.
Shule ina majengo yenye viwango na mabweni ya
wanafunzi ya kulala yako katika viwango vya hali ya juu.
Shule ina mabweni ya kike na kiume watoto
huwa wanakutana pamoja jioni
kwenye ”Study room” ambapo pia sehemu hii imejengwa kwa ustadi . Kwakweli
nimeona mabweni mengi lakini mabweni ya shule
ya Mushemba ni mojawapo ya mabweni yenye viwango, kuna usafi wa hali ya juu ,shule
hii hata ukimuacha mtoto ili alale
,unakuwa na amani moyoni kwamba mtoto
umemuacha sehemu salama.. Watoto wana walezi wenye upendo na wanaonekana wako makini sana na kazi
yao.
MADARASA.
Nilipata
muda pia wa kutemebelea madarasa yao
ambayo kwa kweli ni mazuri kama mnavyoona hapo kwenye picha lakini cha msingi ,
ufundishaji mahiri wa walimu ambao wote wanaonekana kuwapenda watoto , hii ni shule inayokazia
walimu kuwa na wito, upendo kwa watoto na kutokimbilia adhabu zinazowaathiri watoto
kisaikolojia.
Baada ya hapo nilihudhuria sherehe ya kuwapongeza watoto walioshinda,Kulikuwepo
na nyimbo, watoto waliimba na kuonyesha vipawa vyao , maigizo na chakula kizuri.
Baba
Askofu Dk. Samson Mushemba ambaye ni mlezi wa shule hii, naye alihudhuria
sherehe hii na aliwaasa watoto kusoma kwa bidii na kutanguliza heshima na adabu kwa walimu wao.
Itakumbukwa kwamba , pamoja na shule kufanya vizuri, shule hii inasaidia na
kusomesha watoto wanaotoka kwenye
mazingira magumu , wengi wao wakiwa wamefiwa na wazazi mmoja au wote wawili na wanafunzi wengine ni
wale wenye uwezo wa kulipa ada wenyewe.
Asilimia 50 ya watoto wanaosoma katika
shule hii , ni wale wanaolipiwa ada na asilimia 50 ni wale wenye uwezo wa
kulipa ada wenyewe.
Maono ya shule hii , pamoja na kwamba imeendelea kufanya vizuri, kiwilaya , kimkoa
na kitaifa, ni kuendelea kuwasaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu kwa
njia hii pia ni kuendelea katika
kusaidia juhudi za serikali ya mheshimiwa
Dr. John Pombe Magufuli katika kuwawasidia wanyonge kuwapa elimu bora.
Nikiwa naelekea nyumbani nilienda
natafakari , hakika tunahitaji
shule za namna hii nyingi zenye ubora lakini pamoja na ubora wa hali ya juu bado shule ina nafasi kwa watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu!
Kweli kuna umuhimu wa shule
nyingine kwenda kujifunza jambo hili katika shule ya Mushemba! Kweli
shule hii ni bora .
Baba askofu mstaafu Dr.Samson Mushemba akitoa neno katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi wa darassa la nne shule ya Mushemba Trinity school
Kwa maelezo zaidi kuhusu shule hii na uwezekanao wa kupata nafasi ya mtoto wako.
piga simu
namba 0754 9060183 au 0788 819 725
Email. mushemba.found @gmail.com
Muonekano wa mazingira na Majengo ya Shule hiyoMuonekano wa mazingira na Majengo ya Shule hiyo
Utaratibu wa kukabidhi zawadi kwa Wafanyakazi wa shule hiyo ukiendelea
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Mwl Johansen Jonadhan akipokea mkono wa pongezi na zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule ya Mushemba Trinity Bw. Josephat Mushemba kufuatia kazi nzuri wanayoifanya.
Mkurugenzi wa Shule ya Mushemba Trinity Bw.Josephat Mushemba akikabidhi zawadi kwa kwa Mwalimu Gilbert.
Muendelezo wa mtukio ya picha wakati Mkurugenzi wa Shule ya Mushemba Trinity Bw. Josephat Mushemba akiwakabidhi zawadi Walimu wote wa Shule hiyo na wafanyakazi wote wa Idara mbalimbali shuleni hapo kufuatia kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kuifanya.
NOTE:Kwa maelezo zaidi kuhusu shule hii na uwezekanao wa kupata nafasi ya mtoto wako.Wasiliana nao kupitia simu namba 0754 9060183 au 0788 819 725
Email. mushemba.found @gmail.com