Bukobawadau

FUTARI MAALUM ILIYOANDALIWA NA RAHYM KABYEMELA KUTOKA SHULE YA MGEZA VIZIWI

Kutoka Viwanja vya Shule ya Msingi Mgeza Viziwi Manispaa Bukoba,Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro ,Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta na Mhashamu Baba Askofu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki la #Bukoba Siku yajuzi waliweza kuhudhuria hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na Mr Rahym Kabyemela kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa usikivu na wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) pamoja na wenye mahitaji maalum.
Mbali na futari hiyo pia familia ya Mwalimu Amini wa Mugeza Viziwi imetumia nafasi hiyo kuwaaga rasmi wanafunzi na watumishi wa taasisi Mugeza Viziwi kufuatia kustaafu kwake kwa mujibu wa Sheria.
Baadhi ya wanafunzi wa Mugeza Viziwi na Mugeza Mseto walioshiriki futari hiyo.
 Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa shule ya Msingi Mgeza Mseto
Familia ya Rahym Kabyemela ikiwa tayari kwa ajili ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya makundi ya watoto wenye uhitaji ikiwa ni muendelezo wa kusaidia jamii iliyowazunguka
 Wakati wa Swala ya magharibi
Ndugu Rahym Kabyemela wakati akisalimiana na Waalikwa
 Sheikh Haruna Kichwabuta na Sheikh Kakwekwe wakimpokea mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro ambaye pia ni mwakilishi wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti
 Bwana Jamal Kalumuna akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta
 Weldone Ndugu Rahym Kabyemela kwa kuwakumbuka watoto hawa,God Will bless you always!!
 Anawasili Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mahala hapa
 Waalikwa wakiwa tayari kushiriki futari hiyo
Bi Shamila Mkude akiwajibika kuwasogezea huduma watoto wenye ulemavu
Manshallah!Mwenyezi mungu akuzidishie wewe  na familia yako kwa upendo huu.
Mtoto Ilhas Rahym akikata Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kushiriki futari na watoto wenzake wenye mahitaji maalum
 Wanafunzi wakiwa tayari kwa ajili ya Iftar iliyoandaliwa na familia ya Rahym Kabyemela
Harlon Baruti katika utaratibu wa kuwapatia watoto Keki ikiwa ni Ishara ya Upendo kwa watoto hao
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akiongoza utaratibu wa kuwapatia Keki wanafunzi hao
Muonekano wa watoto hao wenye ulemavu wa usikivu na wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) pamoja na wenye mahitaji maalum wakiendelea kupata futari iliyoandaliwa na Rahym Kabyemela.
Wanafunzi wakibata futari iliyoandaliwa kwa ajili yao katika Viwanja vya shule ya Msingi Mgeza Viziwi
Wakati watoto hao wenye ulemavu wa usikivu na wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) pamoja na wenye mahitaji maalum wakiendelea kupata futari iliyoandaliwa na Rahym Kabyemela.
Naam!
 Waalikwa wakiendelea kupata futari

Watoto hao wenye ulemavu wa usikivu na wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) pamoja na wenye mahitaji maalum wakiendelea kupata futari iliyoandaliwa na Rahym Kabyemela.
Viongozi na watumishi wa Shule ya Msingi Mgeza Mseto wakipata futari
Sheikh Haruna Kichwabuta akiongoza wageni mbalimbali na Viongozi wa Vyama na Serikali kupata futari
Taswira mbalimbali katika picha wakati Utaratibu ukiendelea
 Mhashamu Baba Askofu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki la #Bukoba akitoa neno katika shughuli ya futari iliyoandaliwa na Rahym Kabyemela kwa ajili ya watoto wenye uhitaji
 Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna kichwabuta akitoa nasaha zake pamoja na kumshukuru Rahym Kabyemela
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro akitoa neno
 Meya Manispaa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kahororo Chief Kalumuna
 Sehemu ya wadau waalikwa pichani
 Mwalimu Amin ambaye ni mstaafu wa Shule ya Msingi Mgeza akitoa neno na utambulisho kwa familia yake
 Aliyesimama ni Mke wa Mwalimu Amin wakati wa utambulisho
Pichani ni watoto wa Kuzaliwa na Mwalimu Amin
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mganyizi Zachwa akitoa neno
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Willy Mtabuzi akitoa salaam zake kwa waalikwa
 Wilbroad Mtabuzi MNEC Mkoa Kagera akiendelea kutoa neno
 Meya Chief Kalumuna na Mnec Wilbroad Mtabuzi wakibadilishana mawazo
 Bwana Mwilima pichani akifuatilia kinachojiri
Muendelezo wa Matukio ya picha.
 Bwana Hamza Ngemera Itembwe akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao
 Katika picha ya pamoja
 Viongozi na waalikwa katika picha ya pamoja na wanafunzi hao
 Matukio ya picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
 Sheikh Norman mratibu wa shughuli nzima akiendelea kuwajibika
 Hakika mwenyezi aendelee kuibariki i Bukoba, tuzidishie upendo, ushirikiano na mshikamano kwa maslahi mapana ya jamii yetu na Taifa kwa ujumla
 Muendelezo wa matukio ya picha.
Mwishi #Bukobawadau tunawatakia muendelezo mwema wa mfungo wa Ramadhani!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau