WALIOMCHOMA MOTO BINTI HADI KUFA KORTINI!
: Watu 16 wameshtakiwa nchini Bangladesh kwa mauaji ya kushtua ya binti aliyechomwa moto hadi kufa baada ya kutoa taarifa ya kufanyiwa udhalilishaji wa kingono.
Kabla ya kutekelezwa kwa unyama huo, binti Nusrat Jahan Rafi, aliyekuwa na miaka 19, alidaiwa kunyweshwa mafuta ya taa na kisha kulipuliwa moto akiwa juu ya paa la shule ya Kiislamu Aprili 6, zikiwa zimepita siku kadhaa tangu awasilishe malalamiko yake polisi.
Miongoni mwa waliokuwa wametajwa kwenye madai hayo alikuwa ni mkuu wa shule, Siraj Ud Doula, ambaye pia amejumuishwa katika kesi hiyo.
Polisi nchini humo wamesema, mkuu huyo alitoa amri ya binti huyo kuuawa akiwa jela iwapo hatafuta madai yake hayo dhidi yake.
Aprili 6 binti huyo alihudhuria darasani kwaajili ya mitihani yake ya mwisho na ndipo ilipodaiwa alipotelea darini na kisha kuwashwa moto na kundi la watu waliokuwa wamevalia mavazi aina ya burka (mavazi ambayo huziba uso na mwili mzima).
Taarifa zaidi za polisi zimedaiwa kuwa mpango huo uliandaliwa ili uonekane kama amejiua mwenyewe, lakini bintiI huyo aliyekuwa ameungua kwa asilimia 80 aliweza kutoa maelezo yake kabla ya kufariki dunia Aprili 10.