KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AWASILI MKOANI KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA
Na: Sylvester Raphael
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya kitengo cha UKIMWI inayotoa huduma kwa wananchi na kufadhiliwa na nchi ya Marekani.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya kitengo cha UKIMWI inayotoa huduma kwa wananchi na kufadhiliwa na nchi ya Marekani.
Kaimu Balozi Dk. Patterson akiongea na Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ofisini kwake mara baada ya kuwasili Juni 10, 2019 mkoani Kagera alitoa pole kwa wananchi wa Manispaa ya Bukoba waliokumbwa na mafuriko Mei 26, 2019 na kusema kuwa aliguswa na tukio hilo lililoleta taflani kwa wananchi aidha aliishukuru Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa kwa hatua zilizochukuliwa haraka kunusuru maisha ya wananchi hao.
Akitaja dhumuni la ziara yake mkoani Kagera Kaimu Balozi Dk. Patterson alisema kuwa amekuja Kagera kuona mafanikio ya miradi ya maendeleo hasa Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Marekani kwani mkoa wa Kagera unaonekana kunafanya vizuri hasa katika upimaji wa watu waliombukizwa na Virusi Vya UKIMWI (VVU) hasa wananume, utoaji wa dawa za kufubaza nguvu za Virusi, pia wananchi kuhamasika kupima katika vituo vya afya.
“Nimefurahi sana kufika hapa kujionea miradi tunayoifadhili lakini kikubwa na nia yangu ni kuona maambukizi ya VVU yanashuka pia mkoa huu umebarikiwa kuwa na chakula cha kutosha lakini inaonekana udumavu wa watoto bado ni mkubwa lazima kuangalia mbele kwanikwa takwimu za sasa idadi ya watu Tanzania ni karibu milioni 60 lakini lazima tufikirie mwaka 2045 wingi huo wa watu utakuwa mara mbili yaani milioni 120 lazima tuanze sasa kujenga kizazi chetu. “ Alisisitiza Kaimu Dk. Balozi Patterson
Naye Mkuu wa Mkoa Gaguti akimweleza Balozi Dk. Patterson juu ya namna mkoa unavyopambana na udumavu alisema kuwa kwa Kagera chakula si tatizo bali elimu tu kwa wananchi ambapo alisema kuwa sasa udumavu imekuwa ajenda yake na ya mkoa mzima kwa kutoa elimu juu ya lishe bora kwa wananchi ili kuhakikisha tatizo la udumavu linaondoka katika mkoa wa Kagera.
Naye Mgagnga Mkuu wa Mkoa Dk. Marco Mbata katika mazungumzo hayo alimhakikishia Kaimu Balozi Dk. Patterson kuwa takwimu za hivi karibuni za udumavu kwa mkoa wa Kagera umeshuka kutoka asilimia 41.7 hadi asilimia 39.8 na mkoa bado unaendelea na kutoa elimu kwa wananchi lishe bora kwa kutumia vyakula mbalimbali vilivyomo mkoani Kagera badala ya kula chakua aina moja tu ndizi.
Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti alimweleza Kaimu Balozi Dk. Patterson juu ya fursa mbaimbali za uwekezaji kama kilimo, ufugaji, utalii na nyinginezo ambapo alisema katika sekta ya kilimo mkoa una eneo la kilimo na kuna fursa kubwa ya kilimo cha Vanila. Aidha, zao la kahawa mkoa wa Kagera unazalisha karibu nusu ya uzalishaji wa nchi nzima ya Tanzania na alimwomba Kaimu Balozi kuwaleta wawekezaji kuja kuwekeza katika Sekta hizo.
Akiongelea fursa za uwekezaji Kaimu Balozi Dk. Patterson alisema kuwa mkoa wa Kagera ni kitovu cha usafirishaji kwani mkoa huo umepakana na nchi nyingi ambazo ili kufikika lazima upite Kagera pia Balozi huyo wa marekani alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye uwezo usiokuwa na ushindani kutokana na raslimali ilizonazo kwahiyo wananchi wake hawapaswi kuwa masikini.
Katika Hutua nyingine Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alimpokea ofisini kwake Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania Balozi Yonas Yosef Sanbe ambaye naye aliwasili mkoani Kagera Juni 10, 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Katika picha ya pamoja