KANYIGO MUSLIM SEMINARY WAMSHUKURU MBUNGE WA NKENGE BALOZI DR KAMALA
#Kanyigo #Missenyi
Uongozi wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary iliyopo Kanyigo Wilayani Missenyi wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi dkt Kamala kwa msaada wa Saruji mifuko 100 na namna anavyopokea na kuzishughulikia changamoto zinazowakabili.
Akizungumza wanafunzi na viongozi wa shule hiyo Mbunge Balozi dkt Kamala amesema kuwa ameamua kutoa mifuko mia moja (100) ya Saruji kwa shule zote za sekondari jimboni kutokana na kutambua muhimu wa miundombinu bora katika kuchochea ukuaji wa taaluma na ufaulu wa wanafunzi shuleni.
Balozi dkt Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akiongea na wanafunzi pamoja na Uongozi wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary.
Muonekano wa Jengo la Walimu wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary iliyopo tarafa ya Kiziba Wilayani Missenyi
Uongozi wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary iliyopo Kanyigo Wilayani Missenyi wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi dkt Kamala kwa msaada wa Saruji mifuko 100 na namna anavyopokea na kuzishughulikia changamoto zinazowakabili.
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Kiislam Kanyigo inayotoa Elimu kwa wanafunzi wa Jinsia zote
Wanafunzi wakimsikiliza Mbunge Balozi dkt Deodorus Kamala
Muendelezo wa matukio ya picha #Ziarayabalozikamala #Kanyigo
Wafanyakazi Idara mbalimbali wa Shule ya Kanyigo Muslim wakitoa utambulisho
Viongozi wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary pichani kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shule Hajji Abas, Mzee Anas Muhamad (Mjumbe wa bodi),Mzee Nuru Nyaigesha Mwenyekiti wa Bodi na Sheikh Swaibu ambaye ni Sheikh wa Mtaa wa Kanyigo
Bwana Saidu Kyagulani Msemaji wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge akitoa salaam kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Kanyigo Muslim Seminary pichani kulia ni Joansen Kalokola Kato (Katibu wa Mbunge) na kushoto kabisa ni Mwalimu Mbaraka Rusheke wa shule ya Kiislam Kanyigo.
Bango la Shule ya Kantigo Muslim Seminary inayotoa elimu kwa wanafunzi wa jinsia zote.